Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani akielezea
kuhusu utendaji wa bohari hiyo pamoja na changamoto mbalimbali
wanazokumbana nazo, zikiwemo za vyombo vya dola kuwafumbia macho baadhi
ya wafanyabiashara wanaouza dawa za serikali kiholela pamoja na
wanaokamatwa kwa kutorosha dawa hizo nje ya nchi. Taasisi zilizomwagiwa
lawama hizo ni baadhi ya maofisa kutoka vyombo vya dola, serikalini na
wafanyabiashara. Mwaifwani alidokeza hayo wakati wa Kongamano la Nane la
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) la kujadili tafiti z\ilizofanywa
na wanahabari kuhusu matumizi ya fedha zinazochangwa na wananchi kwa
ajli ya masuala ya afya katika halmashauri 26 nchini.
Meneja wa
Ufuatliaji wa Mipango Kazi na Mpango Mkakati wa Bohari ya Dawa (MSD),
Cosmas Nalimi akielezea jinsi MSD ilivyojidhatiti kuboresha huduma
nchini, wakati wa Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) la kujadili tafiti zilizofanywa na wanahabari kuhusu matumizi ya
fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajli ya masuala ya afya katika
halmashauri 26 nchini. Kongamano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki
mjini Mtwara. Baadhi ya dawa za msd inadaiwa zinauzwa nje ya nchi
ikiwemo Cameroon.
Msajili
wa Baraza la Pharmacy Tanzania, Dk. Midred Kinyara, akielezea mikakati
ya usajili wa maduka ya dawa baridi vijijini wakati wa kongamano
hilo.PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO
No comments:
Post a Comment