KAULI JUU YA MAUAJI YA PADRI EVARISTUS MUSHI
Vijana
wenzangu na wasomaji wa makala. Hivi karibuni kuna vitendo vimeanz
kujijenga katika jamii yetu ambayo haviyoi ishara nzuri tuendako.
Matukio
ya kupigwa risasi padri na kuchomwa makanisa na harakati za muamsho.
Haya yote pamoja na yaliyotokea geita si mambo ya kufumbiwa macho.
Ninaomba niwasihi watanzania wenzangu kuwa haya si mambo
yanayoweza kutuimarisha katika umoja na mshikamano wetu. Niwasihi tena
kukumbuka kuwa umoja na mshikamano wetu haukuja kama ajali ni misingi
ambayo wazee na waasisi wa nchi zetu walikubaliana na kuimarika katika
mioyo yao, tusidharau na wala tusibeze.
Mwisho nirudie kuwaomba
nikiwakumbusha kauli ya Raisi wetu wa jamhuri ya Muungano kuwa "....
Hivi ni vitendo ambavyo sisi wenyewe tunavipanga. Ni jukumu letu
viongozi wa dini,wanaharakati na wanasiasa kukemea haya. Endapo tutaamua
kukemea haya kwa vitendo havitaendelea."
Poleni sana waumini wa dini kwa kupoteza kiongozi wenu nami naungana nami katika kuomboleza na NINALAANI kitendo hiki.
No comments:
Post a Comment