Makamu wa
kwanza wa rais wa Serikali ya Umoja wa kitaifa ya Zanzibar, Seif
Shariff Hamad, amemtangaza Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim
Lipumba kuwa mgombea wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao.
Aidha CUF
imewatangazia neema Watanzania kuwa endapo itachukua madaraka katika
uchaguzi huo itawajaza fedha mifukoni ikiwa ni njia mojawapo ya
kuwaondolea umasikini.
Makamu
huyo wa kwanza wa rais alisema hayo katika mkutano wa uzinduzi wa
oparesheni ya mkachamchaka kuelekea mwaka 2015 (V4C), uliofanyika katika
viwanja vya shule ya msingi Kiwanja cha Ndege, manispaa ya Morogoro.
Alisema
Profesa Lipumba bado ni kiongozi shupavu anayestahili kugombea wadhifa
huo kupitia CUF katika uchaguzi ujao kwakuwa anakubalika ndani ya chama
hicho pamoja na kwa wananchi.
Alisema
kuwa operesheni za V4C zilizoanza Mei mwaka jana zitaendelea nchi nzima
kwa viongozi wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho na wafuasi wake
kupita kila kata na wilaya mbalimbali wakihamasisha wananchi kukiunga
mkono chama hicho.
No comments:
Post a Comment