WAKATI
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka hadharani majina ya wajumbe wa Tume
ya Taifa ya Kuchunguza Matokeo yaa mwaka 2012 ya Kidato cha Nne jana,
baadhi ya wajumbe waliopewa heshima hiyo ya kusaidia kutafuta sababu za
matatizo ya elimu na jinsi ya kuyatatua, Mbunge wa Kuteuliwa James
Mbatia na Naibu
Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiel Oluoch, wamekataa uteuzi huo.
Mbatia
katika hoja yake kwa waandishi wa habari jana, alisema kwa kuwa hadi
jana hakuwa amepata taarifa ya maandishi kuhusu uteuzi wake, asingeweza
kutamka kama amekubali au la, hadi atakapokuwa amepata maandishi hayo
akisema atakapoyapata ndipo, “nitafanya uamuzi kwa maslahi ya pamoja ya
Watanzania.”
Hata
hivyo, habari za uhakika kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, zilisema Mbatia
alifahamishwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo kwa njia
ya simu afike Ofisi ya Waziri Mkuu achukue barua yake ya uteuzi kama
walivyofanya wajumbe wengine.
Oluoch
alipotafutwa azungumzie uamuzi wake wa kujitoa kwa mujibu wa barua
aliyoiwasilisha Ofisi ya Waziri Mkuu, alisema yuko mkutanoni akaomba
apigiwe baada ya nusu saa na ilivyofanyika hivyo, alikata simu kila
alipopigiwa.....
SOURCE::HABARI LEO ::
No comments:
Post a Comment