RAIS Mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela amepelekea hospitalini kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.
Taarifa kutoka kwa afisa ya Rais wa Afrika Kusini zimesema kuwa uchunguzi huu ni wa kawaida tu.
Kwa
muujibu wa tovuti ya Urais wa Afrika Kusini, Madaktari wanaomfanyia
uchunguzi Mzee Mandela wamesema hakuna haja ya kuwa na tahariku.
Kwa muda mrefu sasa hali ya kiafya ya rais huyo mstaafu imekuwa ni swala la kutia wasiwasi.
Mandela
mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini kwa siku 18 mwezi wa
Desemba mwaka jana kutokana na kutatizwa na mapafu pamoja vijiwe ndani
ya kibofu chake cha mikojo.
Taarifa
iliyoandikwa kwenye mtandao wa Ofisi ya Rais Jacob Zuma zimeeleza kuwa
Mzee Mandela alipelekwa katika Hospitali ya Mjini Pretoria kwa uchunguzi
wa kawaida wa ki-afya.
Taarifa hiyo imeendelea kusima kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutikana na matatizo yanayoambatana na Umri wake mpevu.
Mzee
Mandela alifudumu kama rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 1994 to 1999
na ndiye rais wa kwanza mweusi kuwahi kuitawala nchi hiyo.
Kutokana
na juhudi zake za kupigania demokraisa na kupambana na sera za ubaguzi
wa rangi nchini humo, Mzee Mandela anatambulika kama Baba wa Taifa
nchini Afrika Kusini.
Tangu mwaka 2004 Mzee Nelson Mandela amekuwa hajitokeza hadharani au kushiriki katika shughuli za umma.
No comments:
Post a Comment