Hatimaye jeshi la Polisi linamshikilia mwanaume anayetuhumiwa kumnajisi,
kumbaka na kumlazimisha kula mbegu zake za kiume binti yake wa kambo.
Mwanaume
huyo, Adam Tuliani, maarufu kwa jina la Kiredio (37) mkazi wa kijiji cha
Mwandege, Wilaya ya Mkuranga, anadaiwa kumfanyia unyama huo mtoto wake
wa kambo mwenye umri wa miaka tisa .
Akitoa
taarifa hiyo, Kaimu Mkuu wa Kituo cha Polisi Vikindu, Inspekta wa Polisi
Bahati Ponela alisema kupatikana kwa mtuhumiwa huyo kunatokana na
juhudi zilizofanywa na Mkuu wa kituo hicho, Inspekta Joseph Ndifwa na
wananchi wa eneo hilo.
No comments:
Post a Comment