Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, May 18, 2013

HOFU YATANDA BUNGENI KUTOKANA NA TETESI ZA SHAMBULIO LA KIKAGAIDI MJINI DODOMA.


Spika wa Bunge Anna Makinda akiingia Bungeni mjini Dodoma kuendesha kikao cha Bunge siku za hivi karibuni.
DODOMA. 

HALI ya wasiwasi imelikumba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kuwepo kwa tetesi ya shambulio la kigaidi katika maeneo ya Bunge.

Hali hiyo inafuatia ujumbe mfupi wa maneno uliosambazwa, ukitaadharisha kuwa kuna tuk

io la kigaidi limepangwa kufanywa katika eneo la Bunge.

Ujumbe huo uliosambazwa kwenye simu za baadhi ya wabunge ulisomeka hivi:-

"Kuna kikundi kina mkakati wa kufanya shambulio la bomu bungeni Dodoma na msikiti wa Msamvu Morogoro. 

Ni ndani ya muda mfupi wakati bado vikao vya Bunge,"ailisema sehemu ya ujumbe huo.

Habari zaidi zinasema kuwa tayari jeshi la polisi imefanikiwa kupata mtu aliyetuma ujumbe huo, ambaye anadaiwa kutuma kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini na wamefanikiwa kumleta mjini hapa kwa mahojiano zaidi ili kufanikisha upelelezi.


No comments:

Post a Comment