Habiba
Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto ni la aibu kubwa
hivyo halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka hatua za
haraka zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida mtoto mwenye umri wa zaidi ya miaka miwili
amefungiwa ndani na wazazi wake kwa kipindi cha miaka miwili sasa bila
kutoka nje pamoja na kukosa matunzo muhimu hali ambayo imepelekea mtoto
huyo kudhoofu kiafya.
Tukio
hilo limetokea leo jijini mbeya katika mtaa wa Ikuti kata ya Iyunga
ambapo majirani wa karibu na mtoto huyo pamoja na baadhi ya viongozi wa
mtaa huo kufika nyumbani anapoishi mtoto huyo kwa lengo la kufahamu
maendeleo yake .
Mtoto
huyo amefahamika kwa jina la Joshua Joseph umri unao kadiriwa kuwa ni
kati ya miaka miwili au mitatu ambaye alikutwa nyumbani hapo akiwa
pekee yake huku wazazi wake wakiwa wameondoka kuelekea kwenye shughuli
zao.
Akizungumzia
tukio hilo Kaimu barozi wa mtaa huo wa Ikuti Ndugu Aloni Mboya amesema
kuwa hali hiyo imenza kujitokeza kwa kipindi cha miaka mitatu sasa hali
ambayo imepelekea mtoto huyo kukumbwa na maradhi ya utapiamlo.
Amesema
katika kipindi cha mwaka 2011 mwezi wa tatu alipokea taarifa kuhusiana
na suala hilo ambapo baba wa mtoto huyo ndugu Joseph Simoni aliitwa
katika ofisi za mtaa kwa lengo la kumhoji juu ya malezi ya mtoto huyo.
Aidha
baada ya kuhojiwa alikiri kosa ambapo alipewa onyo na viongozi wa mtaa
ambao walimtaka kuhakikisha anamtunza vema mtoto huyo kwa kumpatia
chakula bora pamoja na huduma nyingine.
Mara
baada ya mtu huyo kupewa kalipio na viongozi wa mtaa hali hiyo
iliendelea tena ambapo wao kama viongozi wa shina pamoja na wananchi
walimuita yeye pamoja na mke wake aitwaye Sekera Watsoni (40) kuhama
mtaani hapo kwa kwa kipindi cha miezi sita ambapo walikaidi agizo hilo.
Amesema
mara baada ya watu hao kugoma waliamua kuwaacha na kuwaondoa katika
umoja wa ubarozi wao na kuto watambua tena kama wananchi wa eneo hilo
kutokana na vitendo vyao vya kikatili dhidi ya mtoto huyo.
Kwa
upande wao Maafisa maaendeleo ya jamii kata ya Igawilo na Iyunga ambao
ndio waliofika katika eneo hilo wamesema kuwa matukio kama hayo yamekuwa
yakijitokeza mara kwa mara ndani ya jamii hasa kwa vitendo vya
kunyanyaswa kwa watoto wanawake.
Mmoja
wa Maafisa hao Ndugu Habiba Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa
ndani mtoto ni la aibu kubwa hivyo halipaswi kufumbiwa macho na jamii
husika hivyo ametaka hatua za haraka zichukuliwe ili kuokoa maisha ya
mtoto huyo.
Amesema
hali ya kiafya ya mtoto si ya kulizisha kutokana na kusumbuliwanna
maradhi mbalimbali yanayotokana na kukosekana kwa lishe bora pamoja na
huduma nyingine.
Amesema
anawashukuru majirani pamoja na viongozi wengine wa serikali ya mtaa
ambao wamekuwa karibu na mtoto huyo kwa kipindi chote cha miaka miwili
licha ya kutokuwepo kwa ushirikiano toka kwa wazazi wa mtoto ambaye kwa
sasa amefikishwa katika kituo cha afya Inyala Kata ya Iyunga jijini
hapa.
Awali
inaelezwa kuwa baba na mama wa mtoto huyo wamekwisha tengana kwa
kipindi kirefu sasa kutokana na kutokuwepo kwa maelewano ndani ya nyumba
hiyo hali ambayo ilimfanya baba huyo kuoa mwanamke mwingine ambaye
ndiye anaye ishi na mtoto kwa sasa kama mama wa kambo.
Amesema
kutoka na kuwepo kwa mgawanyiko huo ndani ya familia baba pamoja na
mama huyo ambaye ni mke wa pili walichukua jukumu la kuishi na watoto
wote walio achwa na mwanamke wa kwanza ambapo kwa asilimia kubwa ndiko
kuliko sabababisha kuwepo kwa hali hiyo ya manyanyaso ya mtoto.
Hata
wakati wa tukio hilo la kumtoa mtoto huyo ndani baba mzazi wa mtoto
hakuwepo katika maeneo hayo ya nyumbani ambapo maafisa ustawi wa jamii
pamoja na majirani waliamua kuchukua jukumu la kumpeleka mtoto huyo
katika kituo cha afya Inyala kilichopo Kata ya Iyunga kwa lengo la
kumfanyia uchunguzi na kutambua nini kinacho msumbua mtoto huyo.
Picha na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment