MTAYARISHAJI na mwigizaji wa filamu Swahiliwood Isike Samwel akiwa na
rafiki yake Dennis David ambaye pia ni mwigizaji wa filamu Bongo
walijikuta wakinusurika na ajali mbaya maeneo ya Sinza Afrika sana
wakiwa katika gari yake Isike, wakiwa katika barabara inayotokea Polisi
mabatini walipoingia barabara ya Afrika sana waligongwa na gari
iliyokuwa ikija kwa kasi.
.
.
Isike akiongea na FC alisema kuwa kabla ya ajali amekuwa akisakamwa na
maneno ya vitisho kutoka kwa wasanii wenzake wa Bongo Movie wakimuombea
mabaya kwa sababu ya umri wake mdogo wa kufanikiwa kununua gari katika
kazi ya filamu na kuwa na mkataba na kampuni moja ya usambazaji, Isike
amedai kuwa anamshukru Mungu kuepuka na janga ambalo alilihisi awali.
“Ndugu mwandishi namshukru Mungu kwani hadi sasa dua mbaya zimeniandama
kutoka kwa wasanii wenzangu, kwa mfano kuna msanii siwezi kumtaja kwa
jina yeye alimfuata rafiki yangu ambaye ni Editor akimwambia mimi ni
mwanafunzi wake alafu nimenunua gari nitakufa kama
Sharomilionea,”anasema Isike.
.
.
Msanii huyo amesema toka kununua gari hiyo Vitz mayai imemsababishia
maadui ambao ujifanya ni marafiki lakini unapogeuka tu na kuwapa kisogo
umsema vibaya na kumuombea mabaya ikiwa ni kumwona akishindwa kumiliki
gari na kuliuza na kubaki hana kitu, huku akisema sababu kuu, ni yeye
kumiliki gari wakati wasanii wengine wakiwa hawana kitu.
Isike ameusisha ajali yake na imani za kishirikina kwa sababu wasanii
wenzake wamekuwa wakimtishia maisha kwa kutumia nguvu za giza
CHANZO FILAMU CENTRAL





No comments:
Post a Comment