DK 9 Sasa konaaaaaaaa erasto nyoni kapiga mpira uleeee
Kipindi kinaanza ni dk ya 3
Mpira ni mapumziko. Tanzania 2-3 Ivory Coast
Zinaongezwa dakika 2 za nyongeza baada ya dk 45 kuisha.
Toure anapata penati hapa na kuwapatia goli ivory coast
ivory coast wanapata penati
thomas Ulimwengu anaipatia Tanzania goli la kusawazisha akimalizia kazi nzuri ya Shomary Kapombe.
Erasto Nyoni anapiga mpira wa adhabu ambao unadakwa kwa ustadi na kipa wa Ivory Coast.
Thomas Ulimwengu anafanyiwa madhambi na Didier Zakora nje kidogo ya eneo la penati.
Timu zote zinashambuliana kwa kasi ingawa washambuliaji wa Stars wanakosa umakini wakikaribia lango la wapinzani.
Dakika ya 28 - Tanzania 1-2 Ivory Coast
dk ya 22 toure anaipatia ivory coast goli la pili
Kalou anaingia kwenye lango la Stara anachezewa faulo nje kidogo ya eneo la penati.
Dakika ya 21 - Tanzania 1-1 Ivory Coast.
Thomas Ulimwengu na Samatta wanaisumbua ngome ya Ivory Coast.
Taifa Stars wanaonekana kutulia sasa na kupigiana pasi makini katika kutaka kuongeza bao lingine.
Lacina Traore anaisawazishia Ivory Coast
Thomas Ulimwengu anaingia vizuri kwenye lango la Ivory Coast anapiga krosi inayookolewa na Didier Zakora.
Stars wanapata kona ambayo haizai matunda. Dk 5 ya mchezo.
Mpira bado haujatulia timu zote zikipoteza mipira kadhaa ingawa Ivory Coast wanafika zaidi kwenye goli la Stars.
Dakika 3 Ivory Coast wanapata kona ambayo inaokolewa na kuwa mpira wa kurushwa kwenye goli la Stars.
Uwanja wote wa Taifa umefurika mashabiki wakiishangilia kwa nguvu Stars.
Dakika ya 1 kiungo Amri Kiemba anaipatia Tanzania bao la kwanza.
Mpira umeanzaa hapa uwanja wa Taifa
Taifa Stars line up: Juma
Kaseja, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin
Yondani, Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto, Salum Aboubakar 'Sure Boy',
Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na Amri Kiemba
Ivory
Coast line up: Barry Boubacar, Boka Arthur, Didier Zokora, Salomon
Kalou, Yaw Gervais 'Gervinho', Gosso Gosso Jean Jacques, Aurier Alain,
Traore Lacina, Yaya Toure, Serey Geoffroy na Bamba Souleman.
No comments:
Post a Comment