
Mtu kati: Lionel Messi alikuwas Senegal kutembelea akademi ya Aspire Academy
bin zubery
MWANASOKA
bora wa dunia, Lionel Messi ametembelea akademi ya Aspire nchini
Senegal ambako kuna mchezaji mmoja chipukizi kutoka Tanzania, Orgenes
Molel. Na
akiwa huko, amesema anaamini kocha mpinzani wake wa zamani, Jose
Mourinho atapata mafanikio Chelsea na ameweka wazi, Mreno huyo ni 'bonge
la kocha'.Mourinho amerejea Chelsea baada ya kumaliza kuitumikia Real Madrid mwishoni mwa msimu uliopita.
Kocha
huyo wa zamani wa Porto na Inter Milan alikuwa maarufu Hispania kutokana
na kukuza upinzani wa Real na Barcelona katika kipindi alichokuwa
akifanya kazi Madrid.

Mapokezi makubwa: Messi amepata mapokezi makubwa Senegal alipokwenda katika kampeni ya kupiga vita Malaria kwa nchi za Afrika


Mafanikio: Mourinho amechukua nafasi ya Rafa Benitez Chelsea

No comments:
Post a Comment