Mtoto wa kike wa Mpiganiaji Uhuru wa South Africa Nelson Mandela anaeenda kwa Jina la Makanziwe Mandela,Juzi aliongea kwa ukali na kutoa tamko juu ya waandishi wa habari waliopiga kambi nje ya hospital ambayo Baba yake kwa sasa amelazwa akipigania maisha yake kutokana na matatizo ya mapafu.....
Hali hiyo imekuja baada ya vituo vya habari kuweka kambi nje kwenye hospital hiyo iliyopo Pretoria.... Makanziwe akiongea kwenye simu kumjuza mwandishi wa habari wa Ikulu kuhusu Hali ya mzee mandela aliongea hivi ''Tunashukuru Mungu baba kwa sasa hali inaridhisha, ni mtu mzima sana lakini Mungu anazidi kutupigania na familia tunaamini atarudia hali yake kama zamani na kujongea na sisi nyumbani....
Akizidi kuongea,ndipo alipofunguka juu ya waandishi wa habari ''Nachukizwa na kitendo hiki cha hawa waandishi wa habari kabisa wanadiliki kuweka kambi nje ya hospital kuripoti hali ya baba yangu,kusema kweli sijapendezwa au kwa kuwa sisi ni waafrika ndio atupaswi kueshimiwa tunapoitaji undani wetu,nimechukizwa sana yani wapo nje kana kwamba wanasubiri kitoke kitu wawe wa kwanza kuripoti...... Alizidi kusema ''Tunahitaji undani wetu kukiwa na jambo lolote familia itawajuza naomba heshima itumike na busara kwajili ya mzee wetu,sidhani kama angekuwa yupo katika hali nzuri angefurahia kuona kitu kama hiki''
Hayo ndiyo yaliyosemwa na Mtoto wa kike mkubwa wa Nelson Mandela..... |
No comments:
Post a Comment