Mganga
Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (kulia) akiwa na
mratibu wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni 2013, Ssebo wakiwaongoza
warembo mara baada ya warembo hao kutembelea hospitali ya Mwananyamala
kwa ajili ya kutembelea wagonjwa na kufanya usafi.
Mganga
Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (katikati) akiwa na
mratibu wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni 2013, Ssebo wakitoa
maelekezo kwa warembo mara baada ya warembo hao kutembelea hospitali ya
Mwananyamala kwa ajili ya kutembelea wagonjwa na kufanya usafi.
Mganga
Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (kulia) akiwagawia
warembo vifaa kwa ajili ya kujikinga na vumbi mara baada ya warembo hao
kutembelea hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kutembelea wagonjwa na
kufanya usafi.
Warembo wajielekezana namna ya kuvaa vifaa vya kujikinga na vumbi kabla hawajaanza zoezi la kufanya usafi.
Mratibu
wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni 2013, Ssebo akiwaongoza warembo
kuchukua vifaa kwa ajili ya kuanza zoezi la kufanya usafi.
Warembo wa Redd’s Miss Kinondoni 2013 wakiwa katika zoezi la kufanya usafi.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (kulia) akiongea na vyombo vya habari.
Mrembo wa Redd’s Miss Tanzania 2012/13 ambaye alitokea Redd’d Miss Kinondoni 2012 akiongea na vyombo vya habari.
Mratibu wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni 2013, Ssebo akiongea na
vyombo vya habari mara baada ya kumalizika zoezi la kufanya usafi.
Bw.
Ssebo alisema kuwa mchakato wa kumtafuta Redd’s Miss Kinondoni umeanza
kwa kishindo ambapo warembo hao ambao walishaanza kambi tokea mwishoni
mwa wiki iliyopita jana waliweza kutembelea hospitali ya Mwananyamala
na kufanya usafi.
Warembo
hao ambao wanajumuisha vitongoji vya Dar Indian Ocean, Sinza na Ubungo
baada ya kufanya usafi hospitalini hapo walijionea hali mbaya
iliyokuwepo pale na kuamua kufanya harambee ya kuchangisha hela kwa
ajili ya kununua vitanda kwa ajili ya akina mama wanaojifungua (delivery
beds).
Harambee
hiyo imepangwa kufanyika siku ya alhamis tarehe 13, katika ukumbi wa
Ambassador kuanzia saa moja jioni huku mgeni rasmi akiwa ni meya wa
Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda.
Warembo hao leo watafanya usafi hospitali ya Sinza na kutembelea mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi.
Mashindano
ya Redd’s Miss Kinondoni yanatarajiwa kufanyika June 21, huku walowa
yamedhaminiwa na Redd’s Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame
Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media
Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, Mrokim
Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO
Blog, DjChoka Blog na Kajunason Blog.
habari na fullshangwe blog
No comments:
Post a Comment