Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, June 19, 2013

RIBERY NA BENZEMA WATINGA KIZIMBANI JANA, NI LILE SAKATA LA KULALA NA KAHABA CHINI YA MIAKA 18!!

Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
LILE SAKATA ambalo lilianza Mwaka 2010 kuwasakama Wachezaji Nyota wa France, Karim Benzema na Franck Ribery, sasa Kesi yake imeenza rasmi Mahakamani Mjini Paris Siku ya jana e wakituhumiwa kumlipa ‘Changudoa’ alie chini ya Umri halali kisheria ili kufanya nae ngono katika Miaka ya 2008 na 2009.
Benzema na Ribery wanatuhumiwa kumlipa Bibi Zahia Dehar, ambae sasa ana Miaka 21 na ambae alizaliwa Nchini Algeria, kufanya nae Ngono wakati akiwa chini ya Umri halali kisheria huko Nchini France.
Huko France, kulipia Ngono kwa Machangudoa si kosa ila kosa ni kufanya kitendo hicho kwa Mtu ambae yuko chini ya Umri halali wa kuwa Changudoa ambao ni Miaka 18.
Hata hivyo yapo mambo ya utata kuhusu Kesi hii ambayo itaanza kusikilizwa Jumanne bila kuwepo Benzema na Ribery Mahakamani kwani Waendesha Mashitaka walimuomba Jaji aifute lakini Jaji akagomea ombi hilo.
Kwa Mfumo wa Kisheria wa France, Waendesha Mashitaka, wanaoiwakilisha Nchi, hufungua uchunguzi na kuteua Jaji atakaeundesha na kadri uchunguzi unavyoendelea Waendesha Mashitaka wanaweza kumuomba Jaji kufuta uchunguzi lakini Jaji anayo haki ya kuamua kuendelea na kuamua Kesi iende Mahakamani.
On trial: Karim Benzema and Franck Ribery are charged with on charges of soliciting the services of an underage prostituteWaendesha Mashitaka walitaka Kesi hiyo kufutwa baada ya kugundua Benzema na Ribery hawakujua kuwa Zahia Dehar yupo chini ya Umri halali.
Wakati Ribery amekiri kutembea na Binti huyo lakini amedai hakujua kuwa yupo chini ya Umri wa Miaka 18 na pia ni Changudoa.
Mwanasheria wa Ribery, Carlo-Alberto Brusa, ameeleza: “Kwa Sheria za France, sio kosa kufanya mapenzi na Mwanamke na hata kumlipa lakini inakatazwa kufanya hivyo kwa alie chini ya Umri halali! Mwanamke huyu alikuwa akizunguka Ulaya na Ndege utajuaje kwamba ni mdogo?”
Benzema amekataa kabisa kuwa na uhusiano wowote na Zahia Dehar.
Inatarajiwa hukumu ya Kesi itatolewa hapo Juni 26 na ikiwa Wachezaji hao watapatikana na hatia wanaweza kufungwa Miaka mitatu na kupigwa Fani Euro 45,000 kila mmoja.
Court appearance: Alberto Carlo Brusa, lawyer of Bayern Munich star Franck Ribery, arrives at the courthouse in ParisMwanasheria akifika mahakamani: Alberto Carlo Brusa, mwanasheria wa nyota wa Bayern Munich,Franck Ribery akifika mahakamani leo jijini  Paris nchini Ufaransa
Jet setter: Zahia Dehar worked as a prostitute when she was underageKahaba Zahia Dehar alianza kazi yake akiwa chini ya umri wa miaka 18 na kuwaponza Ribery na Benzema
Zahia Dehar
Zahia Dehar
Zahia Dehar amesema hakuwaambia wateja wake kuwa ana umri wa miaka 18
Denial: Ribery says he did not know Zahia Dehar was a prostitute, or that she was underage when she was flown to Munich for his birthdayRibery amesema hakujua kama Zahia Dehar alikuwa kahaba wala kama ana miaka chini ya 18
It wasn't me: Benzema denies any liaison with ZahiaBenzema amekataa kabisa kuwa na uhusiano wowote na Zahia Dehar.
source fullshangwe blog

No comments:

Post a Comment