Mkuu wa
mkoa wa Dar es Salaam, SAID MECK SADICK, amesema serikali imechukua
tahadhari zote katika kuhakikisha shughuli zote za wananchi za
kibiashara zinaendelea kama kawaida wakati wa ziara ya rais wa Marekani
Barack Obama.
Aidha mkuu huyo wa mkoa amesema
katika kipindi hicho wafanyabiashara kutoka mikoani na ndani ya jiji
wataendelea kuingiza bidhaa zao katika masoko kama kawaida bila
kuzuiliwa, na kwamba si barabara zote zitakazofungwa na kutolea mfano wa
barabara itakayofungwa kuwa ni barabara ya Nyerere ambayo wageni wengi
hutumia na kwamba ziara hiyo haitaathiri maonesho ya 37 biashara maarufu
kama sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. JULIUS NYERERE.
Rais wa Marekani Barack Obama
anatarajia kuzuru Tanzania siku ya jumatatu ambapo miongoni mwa masuala
atakayoangazia ni pamoja na kuhamasisha demokrasia na kukuza fursa za
kiuchumi.
Maandalizi ya mapokezi ya Rais Obama
yamezidi kupamba moto hasa katika jiji la Dar-es salaam ambapo ndipo
kituo chake cha kwanza kwa rais huyo nchini Tanzania huku suala la usafi
na matengenezo katika barabara nyingi Jijini likionekana kupewa
kipaumbele tofauti na siku zote.
No comments:
Post a Comment