Issakwisa Mponi na Chande Abdallah
NYUMBA iliyogeuzwa danguro la vijana kuvutia bangi na kufanyia ufuska imenaswa maeneo ya Tabata-Shule jijini Dar.
Kwa
mujibu wa wananchi waishio maeneo hayo, wamekuwa wakikerwa na vitendo
vya kifuska vinavyofanyika katika nyumba hiyo inayodaiwa kumilikiwa na
mwanamke aliyefahamika kwa jina la Deograsia Nchimbi.
Baada ya wananchi hao kutoa malalamiko kwa mama huyo mara kwa mara bila mafanikio, waliamua kukitaarifu kikosi kazi cha waandishi wa Global Publishers Ltd ili waweze kufanya kazi yao.
“Kwa kweli tumesema hadi tumechoka huyu mama amekuwa chanzo cha kuharibu tabia vijana wetu, nyumba yake imekuwa kero, tunaomba Global mfanye kazi yenu ya kufichua maovu.
“Ngono zembe zinafanyika waziwazi bila hata ya kificho, hata sijui tunakipeleka wapi hiki kizazi cha sasa!” alisema mkazi wa eneo hilo aliyeomba hifadhi ya jina.
OFM KAZINI
Baada ya kupokea taarifa hizo, kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) inayoendeshwa na Kampuni ya Global, kiliingia mzigoni na kufanya uchunguzi, kilipobaini ukweli ndipo kilipolitaarifu Jeshi la Polisi, Buguruni kisha kuvamia.
Kikosi kazi cha OFM na polisi walivamia katika nyumba hiyo hivi karibuni majira ya saa kumi na mbili jioni na kuwakuta vijana hao wakiwa na bangi lakini mama mwenye nyumba hakukutwa na kidhibiti.
Ndani ya nyumba hiyo walikutana na vijana wasiopungua kumi lakini waliposikia mlango unafunguliwa walitimka na kuiacha misokoto ya bangi sebuleni ambapo polisi walifanikiwa kumkamata Amosi Nchimbi aliyedaiwa kuwa ni mtoto wa mama mwenye nyumba pamoja na wasichana wawili.
WAFIKISHWA POLISI
Baada ya purukushani ya hali ya juu kati ya polisi na vijana hao waliodaiwa kugeuza nyumba hiyo kuwa danguro, walifanikiwa kuwatia mbaroni wasichana wawili na mtoto huyo wa mwenye nyumba ambapo hadi OFM inaondoka eneo hilo, iliwaacha polisi wakiwa katika harakati za kuwapeleka watuhumiwa Kituo cha Polisi cha Buguruni.
WANANCHI WACHEKELEA
Wananchi pamoja na diwani wa mtaa huo, Mtumwa Mohamed walifurahi kuona vijana hao wakipelekwa polisi kwani hali hiyo ilikuwa ikiharibu tabia za vijana wao kwa muda mrefu hivyo kuishukuru OFM kwa jitihada zake za kufichua maovu katika jamii.
“Nawashukuru kwa kweli hapa palikuwa ni kama chaka la maovu nadhani sasa hali hii itatulia. Hili eneo lilikuwa linaleta picha mbaya kabisa katika jamii,” alisema Mtumwa.

No comments:
Post a Comment