Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, July 14, 2013

WEKUNDU WA MSIMBAZI TAYARI KUWABURUZA KAHAMA UNITED LEO JIONI, JULIO ATAMBA

Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Wekundu wa Msimbazi Simba, “Taifa Kubwa” jioni ya leo wanatarajia kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Kahama United katika uwanja wa Manispaa ya Kahama mkoani  Shinyanga ikiwa ni muendelezo wa mechi za kujipima uwezo katika ziara yao ya mikoani.
Simba wapo Kahama wakitokea mkoani Katavi ambapo walicheza mechi moja dhidi ya Kombaini ya  Katavi na kushinda bao 2-1, lakini kabla ya kwenda Katavi, ilitokea mkoani Tabora ambapo ilipiga mechi moja ya kirafiki dhidi ya maafande wa Rhino Rangers na kuibuka kidedea kwa mabao 3-1.
Baada ya mchezo wa leo, Simba itaelekea Musoma mkoani Mara ambapo itapiga mechi moja dhidi ya Kombaini ya Musoma jumatano ya julai 17.
Akizungumza na FULLSHANGWE kwa njia ya simu kutoka Kahama, kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kiwhelo “Julio Alberto” amesema maandalzi ya mchezo huo yamekamilika, na wachezaji wote wapo salama salimini wakisubiri muda ufike ili waende uwanjani.
“Kwanza namshukuru Mungu mwingi wa rehema, ametupa uzima hapa Kahama, wachezaji wote na viongozi wapo salama kabasi, tunasubiri muda wa mechi ufike ili tukacheze huko”. Alisema Julio.
SIMBASC3
Picha kwa Hisani ya www.Globalpublisher.infor
Julio aliongeza kuwa kikubwa ambacho mashabiki na wanachama wa Simba wanatakiwa kuelewa kwa sasa ni kuwa benchi la ufundi linaijenga timu upya kwa ajili ya mashindano ya siku zijazo.
“Kila mchezo kwetu ni muhimu sana kwasababu tunautumia kuangalia mabadiliko ya kikosi na mapungufu yako wapi na kuyafanyia kazi, kwahiyo muendelezo huu wa mechi za kirafiki unatupa nafasi ya kujua nini cha kufanya”. Alisema Julio.
Pia kocha huyo msaidizi wa Simba aliongeza kuwa kwa sasa kikosi chao kinaimarika kwa kila mechi, huku kocha mtaalamu, Abdallah King Kibaden Mputa akionesha ufundi mkubwa wa kuwafanyisha mazoezi wanandinga wao na kuwapa vitu adimu kiutalaamu.
“Simba ina kocha mahiri na mtaalamu, Alhaji kibadeni, huyu mwalimu ana mambo adimu sana, lazima niwahakikishie mashabiki wetu kuwa Simba ya sasa iatakuwa tishio na hao mnaowaita wakali waleteni msimu ujao, mtaona shughuli ya Mnyama”. Alisema Julio.
Msimu uliopita Simba walikuwa wanatetea ubingwa wao, lakini waliishia nafasi ya tatu, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na wana lambalamba Azam Fc, na ubingwa ukitwaliwa na wazee wa Uturuki, wazeee wa sambusa, Kwalalumpa Malysia, Dar Young Africans chini ya kocha wake Mholanzi Ernie Brandts.
KIBADENINEW
Picha kwa Hisani ya www.Globalpublisher.infor
Kocha mkuu wa Simba, Abdallah King Kibaden Mputa, msimu uliopita aliibuka kocha bora akiwa na kikosi cha Kagera Sugar, msimu ujao ataiongoza Simba
………
Ili kuhakikisha wanarudisha ubingwa wao, Simba wameanza ziara yao mikoani na wataenda mpaka Kenya  ili kukisuka upya kikosi chao, pia wapo makini sana na usajili na hivi majuzi wamemsainisha mkataba wa miaka miwili alyekuwa mfungaji bora wa michuano ya kombe la Kagame iliyofanyika nchini Sudan , Amis Tambwe ambaye alikuwa anaichezea Vital`O ya Burundi.
Nao Yanga walikuwa na ziara ya mikoani ambapo walianzia mikoa ya Kanda ya ziwa na kucheza mechi mbili za kirafiki kati ya KCC ya Uganda. Mechi ya kwanza walicheza CCM kirumba na kutoka sare ya 1-1 na mechi ya pili walirudiana uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na Yanga kulala kwa mabao 2-1. Mechi ya mwisho walipiga Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora na kutoka suluhu ya bila kufungana na wenyeji wao Rhino Rangers.
Sasa Yanga wapo Dar es salaam wakiendelea na mazoezi kwa uzuri kabisa.
e76dYanga1Picha kutoka maktaba

No comments:

Post a Comment