Drogba amefunga mabao dakika za lala salama Kombe la Emirates l
Walcott akishuhudia krosi yake ikiipa Arsenal bao la kuongoza
Walcott akishangilia na wachezaji wenzake wa Arsenal
Emamanuel Eboue (kulia) alikuwa Nahodha wa Galatasaray ilipomenyana na timu yake ya zamani leo, Arsenal
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alivyokuwa baada ya kipigo
MSHAMBULIAJI
Didier Drogba ameendelea kuwa mwiba kwa Arsenal akikumbushia enzi zake
alipokuwa na jezi ya Chelsea, baada ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa
miaka 35 leo kufunga mabao mawili na kuiwezesha klabu yake, Galatasaray
kutwaa Kombe la Emirates.
Kweli,
ni mashindano ya kirafiki na hayana maana yoyote katika msimu, lakini
lilikuwa kama pigo lingine kwa kikosi cha Arsene Wenger.
Mfaransa
huyo aliwaka ile mbaya kana kwamba mashindano hayo yana maana yoyote.
Alimfokea refa wa akiba, Andre Marriner baada ya refa Jon Moss
kuwazawadia penalti wapinzani dakika 12 kabla ya filimbi ya mwisho
kutokana na Ignasi’s Miquel kumsukuma mshambuliaji huyo wa Ivory Coast.
Drogba alikwenda mwenyewe kupiga penalti hiyo na kumpeleka upande tofauti kipa Wojciech Szczesny na mpira alipoupiga.
Drogba
akafunga tena zikiwa zimesalia dakika nne, baada ya kupokea pasi
ya Wesley Sneijder na kumuacha Per Mertesacker, kabla ya kumtungua tena
Szczesny.
Arsenal ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao katika mchezo huo dakika ya 38, mfungaji Theo Walcott.
Katika
mchezo huo, kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny, Jenkinson, Sagna,
Mertesacker, Gibbs/Miquel dk69, Arteta, Ramsey, Oxlade-Chamberlain,
Cazorla/Zelalem dk61, Walcott na Sanogo/Giroud dk61.
Galatasaray Muslera;
Semih, Riera, Chedjou, Eboue, Melo/Sarioglu dk66, Engin Baytar/Gulselam
dk32,Altintop/Colak, dk45, Amrabat, Elmander/Drogba dk45, Umut
Bulut/Sneijder dk45.
No comments:
Post a Comment