Kiongozi
wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda jana amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa
Morogoro kujibu mashitaka matatu yanayomkabili ambayo ni kutotii amri
halali, kutoa maneno yenye nia ya kuharibu imani za dini na kushawishi
kutenda kosa.
Sheikh
Ponda amefikishwa mjini Morogoro na helkopta ya jeshi la polisi majira
ya saa tano asubuhi chini ya ulinzi mkali ambapo askari waliimarisha
ulinzi kwa muda wote huku kikosi cha kutuliza ghasia FFU wakiwa na
silaha mabomu na mbwa ambapo hali hiyo imesababisha kusimama kwa baadhi
ya shughuli zingine za kiofisi katika ofisi zilizopo jirani na mahakama
ya hakimu mkazi wakati kesi hiyo ikiendelea ...
Akisoma
shataka mbele ya hakimu mkazi Richard Kabate , wakili mkuu wa serikali
kanda ya Morogoro Benard Kongola amedai kuwa shekh Ponda anadaiwa
kutenda makosa hayo matatu Agosti 10 mwaka huu majira ya jioni katika
viwanja vya shule ya msingi kiwanja cha ndege manispaa ya Morogoro.
Katika shitaka la kwanza la shekhe Ponda anadaiwa kutotii amri halali ambapo shitaka la pili anadaiwa
kutoa maneno yenye nia ya kuharibu imani za dini kwa kutoa maneno kuwa
serikali iliamua kupeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu
iliyotokana na gesi kwa kuwaua na kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia
90 ya wakazi wa Mtwara ni Waislamu.
Shitaka la tatu linalomkabili
shekh Ponda ni kushawishi na kutenda kosa ambapo anadaiwa kuwa alitoa
maneno ya ushawishi kwa kuwataka waislaam wasikubali uundwaji wa kamati
za ulinzi na usalama za misikiti kwani zinaundwa na Bakwata ambao ni
vibaraka wa CCM na serikali, na kama kamati hizo zitajitokeza aliwaamuru
wafunge milango na madirisha ya misikiti kuwapiga.
Baada ya
kusomewa mashitaka hayo shekh Ponda anayetetewa na mawakili wasomi
Barthoromew Tarimo na Ignas Punge alikataa mashataka yote matatu na
hivyo upande wa mashitaka kupinga dhamana kwa madai kuwa shekh Ponda
anatumikia kifungo cha nje na kwamba hakutakiwa kufanya kosa, hata hivyo
anakabiliwa na makosa mengine.
Upande
wa mashitaka umedai kuwa upelelezi umekamilika na kesi hiyo itasomwa
tena Agosti 28 mwaka huu ambapo mstakiwa amerudishwa rumande kwa
helkopta jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment