Mkuu
wa Jeshi la Polisi la Tanzania IGP Said Mwema akimkabidhi kitara Mkuu
wa Jeshi la Polisi la Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga kama
ishara ya kumkabidhi uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Polisi Kusini
mwa Afrika (SARPCCO)
baada ya Tanzania kumaliza uongozi wake kwa kipindi cha mwaka
mmoja.Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa mkutano maalumu wa wakuu
hao uliofanyika nchini Namibia.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi,
Windhoek Namibia)
Mkuu wa Jeshi la Polisi
la Tanzania IGP Said Mwema akiongozwa na Askari wa Namibia kuingia
katika ukumbi wa mkutano ambapo alitumia fursa hiyo kukabidhi uenyekiti
wa Shirikisho la wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) kwa Mkuu wa
Jeshi la Polisi la Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga.(Picha
na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
Mkuu
wa Jeshi la Polisi la Tanzania IGP Said Mwema akipokea zawadi kutoka
kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia Luteni Jenerali Sebastian
Ndeitunga baada ya kumkabidhi
uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika
(SARPCCO).(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
………………………………………………………………………..
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi,Windhoek Namibia.
Inspekta
Jenerali wa Polisi wa Tanzania IGP Said Mwema amekabidhi uenyekiti wa
Umoja wa wakuu wa majeshi ya Polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika
SARPCCO baada ya kumaliza kipindi chake cha mwaka mmoja cha kuongoza
umoja huo.IGP
Mwema amekabidhi uongozi huo kwa Inspekta Jenerali wa Polisi wa Nchi ya
Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga wakati wa mkutano mkuu
maalumu wa viongozi hao uliofanyika jana katika jiji la Windhoek na kuhudhuriwa na Wakuu wa Polisi kutoka nchi wanachama pamoja na viongozi mbalimbali kutoka INTERPOL na SADC.
No comments:
Post a Comment