Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, August 23, 2013

Michael Wambura: siwezi kujisafisha na maji taka

wambura Michael1 7d828
Aliyewahi kuwa mgombea wa Uchaguzi Mkuu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliosimamishwa na Fifa, Michael Wambura, amesema hatashiriki tena kwenye uchaguzi ujao wa shirikisho hilo, Oktoba 27. (HM)
Awali Wambura, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa FAT (sasa TFF), aliwania nafasi ya Makamu Rais katika uchaguzi uliosimamishwa na Shirikisho la Soka Ulimwenguni (Fifa), kutokana na kuwepo malalamiko kutoka kwa watu walioenguliwa akiwamo yeye.

Juzi TFF ilitangaza majina ya wagombea 58 wote ikiwa ndiyo siku ya mwisho kurejesha fomu, lakini bila kuwepo kwa jina la Wambura ambaye alipoulizwa na Mwananchi sababu ya kutogombea tena alisema: "Siwezi kujisafisha na majitaka."

"Nimeamua kupumzika, nilipigania haki imepatikana kwa kamati mbili kuundwa. Bila mimi kamati hizo zisingekuwapo, lakini jambo muhimu ni kwamba siwezi kujisafisha na majitaka," alisema Wambura.

"Mfumo wa uongozi TFF ni mbovu, kumejaa siasa za majitaka, hizo kamati zilizoundwa hazitafanya kazi kwa vile tu Wambura hayupo, ningekuwepo zingepata kazi ya kufanya," alitamba Wambura.

Wakati Wambura akiingia mitini, Jamal Malinzi amejitosa tena kuwania nafasi ya Urais akichuana na Athuman Nyamlani, Omari Nkwarulo na Richard Rukambura.

Nafasi ya Makamu wa Rais inawaniwa na Iman Madega, Ramadhan Nasib na Walace Karia, huku wajumbe waliomba kuwakilisha kanda mbalimbali ni Abdallah Mussa, Kaliro Samson, Jumbe Magati, Mugisha Galibona, Vedastus Lufano, Samwel Nyalla, Epaphra Swai, Mbasha Matutu, Stanslaus Nyongo, Ally Mtumwa, Elley Mbise na Omari Walii.
Wengine ni Ahmed Mgoyi, Yusuf Kitumbo, Ayoub Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja, Ayoub Nyenzi, Cyprian Kuyava, David Lugenge, Elias Mwanjala, Eliud Mvela, John Kiteve, James Mhagama, Kamwanga Tambwe na Stanley William Lugenge, Athuman Kambi, Francis Kumba, Zafarani Damoder.

Charles Komba, Hussein Mwamba, Stewart Masima, Farid Nahdi, Geoffrey Nyange 'Kaburu', Riziki Majala, Twahil Twaha Njoki, Davis Mosha na Khalid Mohamed. Alex Kamuzelya, Juma Pinto, Muhsin Balhabou, Omar Abdulkadir, Shaffih Dauda na Wilfred Kidao. Kwa upande wa TPL Board waliojitokeza kuwania uongozi wa juu ni wawili Hamad Yahya (Mwenyekiti) na Said Muhamad Said (Makamu Mwenyekiti).Walioomba nafasi za ujumbe wa TPL Board ni Kazimoto Muzo, Michael Kaijage, Omari Mwindadi, Salum Rupia na Silas Magunguma. Chanzo: Mwananchi

No comments:

Post a Comment