Mshindi
wa taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2012/2013, Hadija Saidi Juma Mswaga,
ambaye pia ni Miss Utalii Morogoro 2012/13, ataondoka nchini 28-9-2013 kwenda
nchini Equatorial Guinea, ambako Fainali za Dunia za Miss Tourism World 2013/14
zinafanyika Tarehe 12-10-2013 katika ukumbi wa kimataifa wa Sipopo Conference Centre Malabo
Equatorial Guinea. Kwa mujibu wa Taarifa iliyo tolewa na Fredy Njeje,
mkurugenzi wa Habari na Masoko wa Miss Tourism Tanzania Organisation (MTTO),
jumla ya washiriki kutoka nchi 126 Duniani watashiriki katika mashindano hayo
ya Dunia,ambayo mwaka Jana yalifanyika nchini Thailand ambapo mrembo
Tatyana Maksimova kutoka nchini Urusi alishinda Taji la Miss Tourism World 2012/13.
Hii
itakuwa ni mara ya nne kwa Tanzania kushiriki mashindano hayo ya Miss Utalii
Dunia, ambapo kila mwaka kuanzia mwaka 2005 tumeshinda mataji, Mataji hayo na
washindi kutoka Tanzania katika mabano ni Miss Tuourism World 2005- Africa
(Witness Manwingi – Tanzania), Miss Tourism World 2006 – SADC (Killy Janga –
Tanzania), Miss Tourism World 2007 – Africa (Lillian Cyprian – Tanzania), Miss
Tourism World 2008- Internet ( Lilly Kavishe – Tanzania) na Miss Tourism Model
Of The World 2006 –Personality ( Witness Manwingi – Tanzania). Tangu mwaka 2008, Tanzania haikushiriki
katika mashindano hayo kutokana na kutokana na kukosa wadhamini wa safari hizo
na matatizo mengine ya kiufundi yaliyo pelekea mashindano hayo kutofanyika
nchini tangu 2008- 2010. Njeje alisema kuwa, Miss Utalii Tanzania 2012/2013,
Hajija Saidi Juma Msugwa, anajukumu zito zaidi ya washiriki wengine wote walio
tangulia kwani anakazi ya kwenda kulinda heshima ya Tanzania na kudumisha
rekodi ya Miss Utalii Tanzania ya kutokushindwa katika mashindano yoyote ya
kimataifa na Dunia.
Nae
Miss Utalii Tanzania 2012/13, Hajija Saidi Juma Mswaga, amesema kuwa anatambua
jukumu kubwa na zito alilonalo la sio kutangaza Utalii na Utamaduni wa Tanzania
tu, bali kulinda heshima ya Tanzania na Mashindano ya Miss Utalii Tanzania ya
kutowahi kushindwa katika mashindano yoyote ya kimataifa. “Nawaomba watanzania
waniombee na kunipa ushirikiano wa hali na mali katika kufanikisha maandalizi
yangu na safari ya kupeperusha bendera ya Taifa katika medani ya kimataifa”. Shindano
la Miss Tourism World 2013, litarushwa na kuonyeshwa LIVE katika nchi zaidi 130
Duniani kote na kushudiwa na zaidi ya watazamaji 650 Milioni Duniani kote, huku
washiriki wakipewa fulsa ya kuonyesha vivutio vya utalii vya nchi zao, kupitia
vyombo mbalimbali vya habari vya Televisheni, Majarida na Mitandao.
Regards
Erasto Gideon Chipungahelo
No comments:
Post a Comment