FILAMU ya Foolish age ya msanii wa kike mwenye mvuto Bongo Elizabeth
Michael ‘Lulu’ imekwama bodi ya ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza
baada ya kukutwa na picha zilizo nje ya maadili ya Kitanzania, filamu
hiyo ambayo ilipanga kuzinduliwa mwezi huu tarehe 30 katika ukumbi wa
Mlimani City inahitaji marekebisho chanzo chetu makini kimebaini.
.
Kikwazo kilichoikumba filamu hiyo ni nguo fupi zilizotumika katika
waigizaji walioshiriki katika filamu hiyo ambayo inatabiriwa kufanya
vizuri katika soko la filamu Bongo kama itafanikiwa kuzinduliwa na
kuingia sokoni, juhudi zinafanyika kuhakikisha kuwa marekebisho
yanafanyika ili kwenda na ratiba kama ilivyopangwa.
Hivi sasa baada ya urasimishaji wa filamu mamlaka na taasisi zinazohusika na masuala ya filamu zimekuwa makini na kuhakikisha kuwa filamu zinazoingia sokoni na zile zinazozinduliwa kukaguliwa kabla ya kufanyika kwa matukio hayo kama ilivyokuwa awali, kama filamu hiyo ya Foolish age itashindwa vigezo vya madaraja yanayotolewa na Bodi hiyo haitaonyeshwa.
Lulu ndio mwigizaji bora wa kike kwa mwaka 2013 kupitia tamasha la filamu la kimataifa la ZIFF katika kipengere cha tuzo za Bongo movie kilichopewa jina la Zuku Bongo movie Awards zilizotolewa katika ukumbi wa Ngome Kongwe.
CHANZO : FILAMU CENTRAL
.
Mwigizaji wa filamu Swahilihood Lulu.
Lulu akiwa katika pozi

No comments:
Post a Comment