Habari toka Kariakoo zikitujuza Uvamizi wa ghafla uliofanywa kwa kushirikisha Polisi na Raia wa Kizungu waliopita kwenye maduka na kuchukua simu zote za aina ya Samsung za kichina.
Baada ya kufanya mahojiano kwa njia ya mtandao na simu na baadhi ya wafanyabiashara, tulifahamishwa kuwa hii ni mara ya tatu na baadhi ya wafanyabiashara wamekiri kuwa huu ni mchezo mchafu unaochezwa na baadhi ya Maaskari polisi wa Kituo cha Msimbazi......"
Kwa masharti ya kutotajwa jina mfanyabiashara mmoja alikuwa na haya ya kusema “yaani hawa wazungu wamevamia hapa na Askari na kuchukua simu za kichina za Samsung wakati sisi mzigo tunanunua china hivi ni halali kweli ? Ujue Watanzania tunashushana na kutiana umaskini wenyewe kwa wenyewe ... hii ni mara ya tatu na kila wakija wanachukua mzigo wote hivi ni kweli serikali haijui ? au mpaka siku tuliwashe ndio watu watafutane au ijulikane? Au wanataka waseme tulianzisha vurugu , Raia wa kigeni aingie duka la mzalendo kupekua kweli jamani? Inauma sana unajua ?
Toka kwa Mdau aliye kula hasara mzigo wa SUMSANG sasa wao wanadai ni SAMSUNG
via Jf
No comments:
Post a Comment