MSHAMBULIAJI
Mario Balotelli amefungiwa mechi tatu kufuata kumvaa refa katika mchezo
ambao timu yake, AC Milan ilichapwa mabao 2-1 na Napoli Jumapili.
Balotelli,
ambaye alikosa na kufunga bao zuri la kufutia machozi kwa timu yake,
alionyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya mechi kwa kumvaa refa.
Mshambuliaji huyo wa Italia sasa atakosa mechi tatu zijazo kwa kosa hilo.
Balotelli,
ambaye alifunga penalti zake zote 21 za awali katika mechi rasmi,
mkwaju wa Jumapili uliokolewa na kipa wa Napoli, Pepe Reina.
Kadi hiyo
nyekundu ya utata, inamaanisha Super Mario atakosa mechi na Bologna,
Sampdoria na Juventus, ingawa Milan inaweza kukatia rufaa adhabu hiyo.
Chanzo: binzubeiry
No comments:
Post a Comment