Mashabiki
wake hupendelea kumuita "King of BongoCrunk"....jina halisi ni Ilunga
Khalifa a.k.a CPwaa! Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania ambaye baada ya
ukimya mrefu sasa kuachia kazi zake mpya.
C.P a.k.a
CPwaa mwenye tuzo 3 za Tanzania Kilimanjaro Music Awards na Multiple Channel O
Africa Music Video Awards nominations anakuja kivingine kabisa mwaka huu.
Tarehe 1 mwezi wa October 2013, CPwaa ataachia single yake mpya na ya kwanza
kabisa kwa mwaka huu.Single hiyo iitwayo "Chereko Chereko" yenye
mahadhi ya AfroDance imefanywa chini ya studio za 'De Fatality Music" na
producer "Mesen Selekta" ambaye mwaka huu alichukua tuzo ya
mtayarishaji bora Tanzania anayechipukia.Nyimbo hii itapatikana kwenye mitandao
yote na media zote kuanzia tarehe moja October.
CPwaa ambaye
amesaini mkataba mnono na Universal Music group vile vile anategemea kuachia
single nyingine mwanzoni mwa mwaka 2014 ambapo amewashirikisha mafahari wengine
wawili kutoka Afrika. Single hiyo ya kimataifa iitwayo "Cross-Borders
Therapy" imekutanisha wakali kutoka mashariki,magharibi na kusini mwa
Afrika. CPwaa amemshirikisha "DBlack" kutoka Ghana, DBlack ni moja ya
wasanii wakubwa wa Hip Hop Afrika ambaye ana tuzo nyingi ikiwemo zile za Channel
O.Kwa upande wa Afrika ya kusini CPwaa amemshirikisha "Hip Hop
Pantsula" a.k.a HHP kwenye nyimbo hiyo hiyo ya Cross Borders Therapy.HHP
ni mmoja ya MaMC wakali kutoka bondeni mwenye tuzo nyingi ikiwemo ya MTV Base.
Nyimbo hii itakuwa ya kwanza Afrika ambayo imekutanisha wakali kutoka mashariki
,magharibi na kusini ( The first East,West and South African Hip Hop
Collaboration in History).Nyimbo hii pia imefanyika chini ya producer Mesen
Selekta pale "De Fatality Music" Studio.
Kifuatacho
baada ya nyimbo hizi kutoka ni video zake ambapo Chereko Chereko itafanyiwa
Tanzania na Cross Border Therapy kufanyika nchini Afrika ya kusini. Kwa wale
mashabiki ambao watakuwa na kiu ya wimbo wa Cross Border Therapy ambao utatoka
mwakani wataweza kuupata wimbo huo kupitia iTunes,Amazon, Spotify na digital
store zingine bila kusahau mtandao wa "The Kleek" kwa wale watumiaji
wa smartphones za Samsung na Androids.
Asanteni
sana na tuendelee kutoa support kwa wasanii wetu na muziki wetu.
No comments:
Post a Comment