MTU
anayetuhumiwa kuwa daktari bandia aliyekamatwa akijiandaa kufanya
upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC leo atapandishwa kizimbani
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya mjini Moshi kusomewa shitaka kwa mara
ya kwanza.
Mtuhumiwa
huyo, Alex Sumni Massawe, alinaswa Septemba 5, mwaka huu majira ya saa 5
asubuhi katika hospitali akidai kuahidi kumfanyia upasuaji mgonjwa
aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa ngozi.
Kabla
ya kukamatwa kwa Massawe, mama mzazi wa kijana aliyekuwa akitakiwa
kufanyiwa upasuaji, Pamvelina Shirima, alikutana na daktari huyo katika
baa maarufu iliyopo eneo la Dar Street na kumtoza sh 200,000 akidai
zitatumika kuharakisha mwanae afanyiwe vipimo vya upasuaji.
Alex
anadaiwa alitaka kumfanyia upasuaji kijana, Makasi Tipesa, mkazi wa
Manispaa ya Moshi ambaye amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi kwa
muda mrefu sasa.
Tukio
hilo lililoongeza hali ya wasiwasi kwa wagonjwa wanaopatiwa matibabu
katika hospitali hiyo lilifanya uongozi wa KCMC kuimarisha hali ya
ulinzi hosptalini hapo huku wagonjwa wakiendelea kupewa tahadhari ya
kuwatumia madaktari wasiofahamika.
Ofisa
Uhusiano wa Hospitali ya KCMC, Gabriel Chisseo, alisema daktari huyo
aliwekewa mtego na uongozi wa Hospitali ya KCMC baada ya baadhi ya
wagonjwa kuripoti kutapeliwa na mmoja wa madaktari ambaye amekuwa
akijinasibu kwamba anafanya huduma hiyo kutokana na wito alionao katika
fani hiyo.
Alisema
mteja wa hosptali hiyo aliyekuwa akitibiwa alitapeliwa na daktari huyo
na baadaye alifanikiwa kukamatwa akiwa wodi ya upasuaji baada ya kupokea
kiasi cha sh 200,000 kutoka kwa Pamvelina Shirima ambaye alimpeleka
mwanae afanyiwe upasuaji wa ngozi.
No comments:
Post a Comment