Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, September 9, 2013

KIWANDA CHA KWANZA CHA KUCHAMBUA TAKA CHAZINDULIWA

taka_f4772.jpg
Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimlaki mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa alipowasili kukagua kiwanda kipya na cha kwanza nchini Tanzania cha kuchambua taka (KIKUTA) kilichopo Gongo la Mboto jijini Dar. (Picha za Zainul Mzige wa Mo Blog).
taka1_69fb3.jpg
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akisalimiana na baadhi ya wakazi wa Gongo la Mboto mara baada ya kuwasili kiwanda cha KIKUTA
taka2_82943.jpg
Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa kuznugmza na wakazi wa Kata ya Gongo la Mboto.
taka3_94bf7.jpg
Mh. Dkt. Huvisa amempongeza Diwani wa Kata hiyo ambaye pia ni Meya wa Halamshauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa kwa jitihada zake za kuhamasisha usafi kwenye Manispaa yake na kuzitaka Manispaa zingine kuiga mfano wa Manispaa ya Ilala ambapo pia amewahamasisha wakazi wa Gongo la Mboto kutunza Mazingira kwa kupanda miti ili kukabiliana na manadiliko ya tabianchi yanayopelekea ongezeko la Joto duniani.
taka4_7f54f.jpg
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa (katikati) akielekea kukagua kiwanda hicho akiwa amembatana na Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (kushoto) pamoja na Afisa Usafishaji wa Manispaa ya Ilala Bw. Samuel Bubegwa (kulia).
taka5_e0129.jpg
Mh. Dkt. Terezya Huvisa akiangalia maji ya michoro iliyopo katika kiwanda hicho inayohamasisha suala utunzaji wa Mazingira majumbani.
taka6_66e5f.jpg
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi kiwanda hapo namna wanavyotengeza Mbolea kwa kutumia taka zilizooza.
taka7_32800.jpg
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akingalia Mbolea iliyozalishwa kiwanda hapo tayari kwa matumizi.
taka8_6bcc1.jpg
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akikagua kifaa kinachotumika kuchambulia taka kwa ajili ya kuzalishwa upya kiwandani hapo.
taka9_fe763.jpg
Mratibu wa Jamii na miradi kutoka Bremen Overseas Research and Development Bi. Larissa Duma (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa (katikati) alipotembelea na kukagua kiwanda cha KIKUTA. Kushoto ni Diwani wa kata ya Gongo la Mboto na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
taka10_4fda1.jpg
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa kwenye picha ya pamoja na Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa pamoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha kuchambua taka (KIKUTA).
Manispaa ya Ilala katika Kata ya Gongo la Mboto imezindua kiwanda cha kuchambua taka chenye uwezo wa kutengeneza Mbolea, Mboji na bidhaa mbalimbali zitokanazo na taka ngumu na nyepesi.
Kiwanda hicho awa kilijulikana kama kituo cha kutupia taka (KIKUTA) ambacho kilijengwa na mfadhili Bremen Overseas Research and Development kutoka Canada.
Kiwanda hicho cha kipekee kimetokana na juhudi za wakazi wa Gongo la Mboto na Kikundi cha Gongo la Mboto Youth Group wakisaidiana na viongozi wao na Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
Kiwanda hicho kitatoa ajira kwa vijana ili kujikwamua kwenye lindi la umaskini.

No comments:

Post a Comment