Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, September 23, 2013

KUNDI LA WANAMGAMBO WA AL-SHABAAB LINA WANAJESHI ZAIDI 8,000 NA HII NI HISTORIA YAKE.

Kiongozi wa kundi la wanamgambo wa al-ShababAl-Shabab, Ahmed Abdi Godane (katikati).

Al Shabaab wakifanya mashambulizi mjini Mogadishu.

KUNDI la wanamgambo wa Kisomali la al-Shabaab, limevamia jumba la kifahari lenye maduka mengi na mikahawa mjini Nairobi nchini Kenya na kufyatua risasi ovyo na kuua makumi ya raia wasio na hatia. 

Al Shabaab ambao makazi yake makuu nchini Somalia, limeweza kuondolewa kutoka miji mikubwa ya Somalia baada ya kuweka mizizi ikiwemo Mogadishu na sehemu zengine za Somalia , ingawa bado linasalia kuwa tisho kubwa kwa kanda nzima wa Afrika ya mashariki na kati. 

Al Shabaab ni nani ?. 
Jina Al-Shabab linamaanisha Kijana kwa lugha ya kiarabu. Kundi hilo liliibuka kama tawi la vijana la muungano wa mahakama za kiislmau ambao baadaye ulivunjika mwaka 2006, wakati ilipopigana na wanajeshi wa Ethiopia waliokuwa wameingia nchini Somalia kuunga mkono serikali iliyokuwa dhaifu.
Kuna taarifa chungu nzima kuhusu wapiganaji wa kiisilamu wanaokwenda Somalia kupigania Al Shabaab.

Kundi hilo limeweka sheria kali za kiisilamu katika maeneo ambayo linadhibiti ikiwemo kupigwa kwa mawe hadi kufa wanawake wanaodaiwa kufanya uasherati pamoja na kuwakata wezi mikono.

Je Al Shabaab linadhibiti sehemu gani ya Somalia ?.
Ingawa kundi hilo limepoteza udhibiti, wa miji mikubwa, bado linakita mizizi katika maeneo ya mashinani.

Lililazimika kuondoka katika mji mkuu Mogadishu, mwezi Agosti mwaka 2011 na pia kuondoka katika mji wa bandarini wa Kismayo mwezi Septemba mwaka 2012.

Kismayo ulikuwa mji muhimu kwa kundi hilo, ambao ulikuwa unawezesha bidhaa kuwafikia wapiganaji wa kundi hilo pamoja na kuwatoza watu ushuru kwa shughuli zao.

Hizi ni silaha za Al Shabaab walizonasa wanajeshi wa AU.

Muungano wa Afrika, ambao unaunga mkono juhudi za majeshi ya serikali, ulisherehekea ushindi huo ingawa al-Shabab hunfanya mashambulizi ya mara kwa mara ya kujitoa mhanga mjini Mogadishu na kwingineko.

Wadadisi wanaamini kuwa al-Shabab limeanza kufanya mashambulizi ya kuvizia baada ya kushindwa na majeshi ya Muungano wa Afrika wanaotumia nguvu dhidi yao.

Lakini linakabiliwa na tisho kubwa kutoka kwa wanajeshi wa Kenya walianza hatarakti zao dhidi ya kundi hilo kuanzia mwaka 2011.

Kenya ilituhumu wapiganaji wa al-Shabab kwa kuwateka nyara wanajeshi wake pamoja na watalii na sasa wamekuwa katika msitari wa mbele kupambana na kundi hilo la kigaidi.

Wakati huo, wanajeshi wa Ethiopia waliweza kukabiliana na wapiganaji hao na kudhibiti miji ya Beledweyne na Baidoa.

Nani kiongozi wa al-Shabab ?. 
Ahmed Abdi Godane ndiye kiongozi wa kundi hilo. Anajulikana kama Mukhtar Abu Zubair, na anatoka katika jimbo la Somaliland.

Kumekuwa na taarifa za mgawanyiko katika kundi hilo, ambazo hata hivyo zinapingwa vikali na kundi lenyewe. 

Inaarifiwa kuwa uongozi wake unapingwa, na wanachama wanaotoka maeneo ya Kusini na ambao ni wengi katika kundi hilo. Inakisiwa idadi yao ni kati ya wanajeshi 7,000 na 9,000.

Bwana Godane huwa haonekani hadharani, Mtangulizi wake Moalim Aden Hashi Ayro, aliuawa katika shambulizi lililofanywa na Marekani mwaka 2008.

Nini uhusiano wa kimataifa wa kundi hilo?Al-Shabab lilijiunga na al-Qaeda mwezi Februari mwaka 2012. Katika ujumbe wa Video, kiongozi wa al-Shabab Ahmed Abdi Godane alisema anaahidi kuunga mkono kingozi wa al-Qaeda Ayman al-Zawahiri.

Makundi hayo mawili yamekuwa yakifanya kazi kwa pamoja, na raia wa kigeni wamekuwa wakiunga mkono kundi hilo, na hata kuwasaidia katika harakati zao za mapigano.

Mwaka jana maafisa wa al-Shabab waliambatana na mtu aliyesema ni mwanachama wa al-Qaeda na kumtambua kuwa raia wa Marekani Abu Abdulla Almuhajir alipokuwa anatoa msaada wa chakula kwa waathiriwa wa njaa.

Maafisa nchini Marekani wanaamini kuwa wapiganaji wa Al Qaeeda ambao hawajahusina sana na mashambulizi nchini Afghanistan na Pakistan kufuatia mauaji ya kiongozi wao, Osama bin Laden, wapiganaji wake wengi wanakwenda kutafuta hifadhi nchini Somalia.

No comments:

Post a Comment