.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kaimu kamanda
wa polisi mkoa wa Dodoma Mrakibu Mwandamizi Damas Nyanda amesema chanzo
cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi hilo lenye namba za
usajili T 433 BLR aina ya Youtong ambaye alishindwa kulimudu na kuacha
njia na kulivaa lori aina ya Layland Daf lenye namba za usajili T 102
CGR likiwa na tela lenye namba za T 928 na kusababisha watu watano
kufariki papo hapo.
ITV ilifika katika eneo la tukio na kuzungumza na
baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo na wamelalamikia uhaba wa vyombo vya
uokoaji ambapo wamesema kama vyombo vya uokoaji vingefika kwa wakati
huenda watu wote wanne waliofariki kwenye lori wangeokolewa.
Nao baadhi ya majeruhi waliolazwa katika hosipitali
ya rufaa ya Dodoma wamesema kabla ya kutokea kwa ajali hiyo dereva wa
basi hilo alikuwa katika mwendo kasi na baada ya kuliona lori hilo
alifunga breki za ghafla na kusababisha basi hilo kulivaa lori hilo huku
mganga mfawidhi wa hosipitali hiyo Dk Mzee Nasoro akasema walipokea
majeruhi 20 na mmoja kati yao amefariki dunia.CHANZO ITV
No comments:
Post a Comment