Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, October 25, 2013

MAJI MACHAFU YANAYOTOKA KWENYE CHEMBA ENEO LA MWENGE YAZIDI KUWA KERO


Baada ya kuripotiwa  Eneo la Mwenge  kwamba mtaa mmoja wapo umegeuka jina na kuitwa Kinyesi Street jambo ambalo lilikuwa haliwafurahishi wakazi wa eneo hilo...

Na pia Baada ya Kuripotiwa katika Mtandao wetu wa Dar es salaam yetu , Bofya hapa kuona ripoti ya Majuzi  Jumapili  hiyo Asubuhi na Mapema Timu ya kuzibua maji Taka ilifika katika eneo hilo na Kuzibua Chemba hizo .. 
kumbe ilikuwa ni Danganya toto mpe pipi atulie kulia au kichwa kinacho uma unakunywa Tembe kisha kinatulia.HABARI NA DAR ES SALAAM YET
Picha hizi zimepigwa Leo zikionesha jinsi Kero hii inavyo zidi shika Kasi ya Ajabu..
 Hili Ni eneo Jipya kabisa ambalo Chemba hii imeachia na kuanza kumwaga maji machafu ...

Exclussive: Tazama Mzee Huyu alicho kifanya huku Chemba moja wapo ikiwa imepita Ndani mweke jirani kabisa na Ghorofa za JWTZ Mwenge.

 Mzee akionesha Jinsi Chemba ilivyo Jaa na ikitaka kuanza kufuka Maji machafu nje...
 Unaweza kujiuliza kwa nini nyumba hii na chemba hii maji hayajai kama ilivyo huko Nje? na kama inavyo onesha hapa?

 Hii ndio Hali halisi , Baada ya kuona kwamba chemba hiyo ya maji taka iliyo ndani kwake na iliyo wasumbua kwa muda mrefu na kusababisha kero , waliamua kujenga bomba ndani na Chemba hiyo  kitu ambacho kilifanyika ni kwamba walitega na kuhakikisha kwamba maji hayo yakifikia sehemu yaanze kutoka nje kama inavyo onekana hapa sasa. Maji yanatoka nje ingawa yanaingia katika Mtaro.

PICHA HIZI ZIMEPIGWA LEO... JE KWELI HAWA WANAFANYA KAZI IPASAVYO?

 Hii ni sura mpya kabisa iliyo jitokeza eneo hili nyuma ya Maghorofa ya Jeshi ambapo sasa Mtaa huu watu wanauita , Mtaa wa Kinyesi unatoa Harufu mbaya sana jambo ambalo limezidi kuwakera wakazi.
 Watu hawa wametoka Dukani na hapa wamekwama kutokana na kwamba hawajui wapite wapi , pamekuwa ni kama mto walichukua zaidi ya dakika tatu huku maji yakizidi jaa.
 Wakati maji machafu yanazidi mwagika kwa kasi ya ajabu , bado kumetokea ishu mbaya zaidi ambapo eneo hili uchafu wa kutosha umekwama, huku Harufu mbaya ikiwa inazidi kutikisa katika eneo hili....

 Huu ni Mtaro ambao kazi yake ni kupitisha maji ya mvua lakini umebadilika na kuwa ndio njia ya haya maji taka...
 Kama katikati ya barabara kuna bwawa tena la maji machafu mwananchi anapitaje hapa?
 Chemba sasa imechachamaa... Harufu inayotoka hapa sio ya kawaida .. uchafu ambao unaweza kusababisha  Magonjwa ya Mlipuko.

 Hii  ndio hali halisi ...... huwezi amini huku sasa ni kijito cha maji taka... 



Picha zifuatazo zilipigwa siku ya Jumatatu baada ya kudanganya wananchi kuwa wamezibua chemba hizo ... 
 
Hii ni moja ya Chemba ambayo ilikuwa inamwaga maji kwa wingi sana ambayo yalisababisha mtaa huo kuonekana kama mto
Hii pia ilikuwa ni Chemba ambayo ilikuwa inamwaga maji machafu kwa wingi lakini kwa sasa hali imekuwa salama baada ya kikosi Cha DAWASCO kushuka na kuja kuzibua ...
 
 Mfereji ambao ulikuwa umejaa maji taka ulivyo kuwa unapitisha maji lakini kwa sasa hali ni safi namfereji huo sasa unaonekana kukauka na hatimaye kusababisha wakazi wa eneo hilo kulala kwa amani bila Harufu mbaya . kwa siku kadhaa
Hili ni Eneo la Jeshi ambapo njia hii mpaka Jumapili 20.10.2013   ilikuwa haifai Maji yalikuwa yakitiririka kwa kasi hali ambayo ilisababisha kero kubwa kwa wakazi wa eneo hilo la Mwenge.. Lakini kama inavyo onekana sasa Hali ni Shwari kabisa na maji yanaendelea kukauka ...

Hili ni eneo Sugu ambalo Maji yalikuwa yakitwaama lakini kwa siku chache  hali ilikuwa ni  Shwari kabisa na kama inavyo onekana yanazidi kukauka..

No comments:

Post a Comment