Mahakama
ya hakimu mkazi imefuta kesi iliyokuwa inamkabili mbunge wa jimbo la
Arusha Goodbless Lema na kudai kuwa upande wa mashitaka hakuwa na nia ya
kuendeleza kesi hiyo.
Aidha kesi hiyo iliyokuwa inamkabili mbunge huyo ilikuwa ni ya uchochezi katika chuo cha uhasibu Arusha ambapo vurugu hizo
zilisababisha chuo hicho kufungwa.
Pia kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa leo mbele ya Hakimu Devotha Msofe wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ili kuweza kuitolea
ufafanuzi zaidi.
zilisababisha chuo hicho kufungwa.
Pia kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa leo mbele ya Hakimu Devotha Msofe wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ili kuweza kuitolea
ufafanuzi zaidi.
Hataivyio
mara baada ya hakimu huyo pamoja na Jopo la mawakili kuingia mahakamani
hapo, Wakili wa Serikali Elianenyi Njiro, aliiomba mahakama kesi hiyo
ifutwe chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya
Jinai, kama ilivyorekebisha 2002.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa upande wa mashitaka uliona hauna haja wala tija ya kuendelea na kesi hiyo lakini pia ni vema kama kipengele
cha sheria kikaangaliwa zaidi.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa upande wa mashitaka uliona hauna haja wala tija ya kuendelea na kesi hiyo lakini pia ni vema kama kipengele
cha sheria kikaangaliwa zaidi.
Pia
mara baada ya ombi hilo mahakama iliridhia na kudai kuwa kuanzia sasa
Mbunge huyo yupo huru kwa mujibu wa kifungu cha sheria.
“kwa
mujibu wa kifungu cha sheria kuanzia sasa Lema upo huru”aliongeza
hivyo. Awali Akisoma maelezo ya awali Julai 10 mwaka huu mahakamani
hapo, Wakili wa Serikali Elianenyi alidai Aprili 24 mwaka huu, Lema
akiwa eneo la Freedom Square la IAA alifanya kosa la uchochezi wa
kutenda kosa kinyume na Sheria ya Kanuni ya Adhabu.
Akifafanua
shtaka hilo, Elianenyi, alidai kuwa Lema aliwaeleza wanafunzi wa chuo
hicho ambao walikuwa wamekusanyika kufuatia kuuawa
kwa mwenzao na watu wasiojulikana kuwa;
kwa mwenzao na watu wasiojulikana kuwa;
Upande
wa mashtaka tayari ulikuwa umewaleta mashahidi watano ambao ni Kamanda
wa Polisi wa Wilaya ya Arusha, Giles Mroto, Naibu Mkuu wa Chuo cha
Uhasibu Arusha, Faraji Kasidi, Inspekta wa Polisi Bernard Nyambalya,
Jane Chibuga na Mwadili wa Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha, John
Joseph Nanyaro.
No comments:
Post a Comment