Marehemu Zakaria Gindu baada ya kujilipua na moto.
Na Daniel Makaka wa Mo Blog Sengerema,
Mkazi
wa kitongoji cha Kijiweni kilichopo kijiji cha Chifunfu kata ya
Chifunfu wilaynia Sengerema mkoa Mwanza, amefariki dunia baada
yakujilipua kwa moto kisha kuungua vibaya na kufariki dunia akiwa ndani
ya nyumba yake.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Mwenyekiti wa kitingoji hicho Bw. Juma Mashauri,
amemtaja aliyekumbwa na mauti hayo kuwa ni Bw. Zakaria Ngindu (36)
mzaliwa wa kijiji cha Mwamanyiri wilaya ya Busega Mkoa wa Simiyu.
Bw.
Mashauri amesema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo Septemba 27 mwaka huu
majira ya saa10 jioni na chanzo cha tukio hilo inaelezwa kuwa ni
kutokana na ugomvi uliokuwa ukiendelea ndani ya nyumba yake na mke wake
alitajwa kwa jina la Veronica Lumanicha mzaliwa wa kitongoji cha NGOMA
‘B’ Kilichopo kijiji cha Nyamatongo Kata ya Nyamatongo wilayani
Sengerema, baada ya kumkuta akiwa na namba za simu ya mkononi ambazo
hazieleweki kuwa ni za nani.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walisema wanandoa hao walikuwa na
ugomvi wa mara kwa mara wakituhumiana kutokuaminiana katika ndoa yao
iliyokuwa imegubikwa na vitimbwi vingi vililosababisha mmoja wa wa
wanandoa hao kushikwa na hasira na kunywa pombe kisha kuchukuwa maamuzi
ya kujiua ili kuondokana na kero hiyo.
Kutokana
na tukio hilo kwa upande wake Katibu wa umoja wa vijana wa chama cha
mapinduzi (CCM) wilaya Sengerema Bw.Benedictor Bujiku aliyekuwa
ameambatana na waandishi wa habari kushuhudia tukio hilo amewaomba
vijana kupenda kujishugulisha na shuguli na kuacha suala la ulevi
unaopelekea kuchukua maamuzi ya kujiua angali taifa bado linawategemea .
Naye
diwani wa kata hiyo ya Chifunfu Robert Madaha amesikitishwa kwa kutokea
kwa tukio hilo na amewataka wananchi kuacha unywaji wa pombe ambao
hauna faida yoyote kwa ujenzi wa Taifa.
No comments:
Post a Comment