Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, October 7, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI


KAMANDA-DIWANI-ATHUMANIKAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  
PRESS RELEASE” TAREHE 07. 10. 2013.
    
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA MICHE YA BHANGI.
MNAMO TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO ENEO LA UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA JULIUS S/O MWAMBENJE, MIAKA 23,  KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA NSALAGA- UYOLE  AKIWA NA BHANGI MISOKOTO 15  SAWA NA UZITO WA GRAM 75. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KWENYE MFUKO WA RAMBO. MTUHUMIWA NI MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

WILAYA YA MBEYA MJINI – KUINGIA NCHINI BILA KIBALI
MNAMO TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 23:30HRS HUKO ENEO LA STENDI KUU JIJI  NA  MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA 1. NYELAKOZI D/O MELANIA, MIAKA 33,,MKULIMA,  NA 2. NDAISHIMILI D/O TEONYA,MIAKA 33,WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI BURUNDI  WAKIWA NA WATOTO 11 AMBAO PIA NI RAIA WA BURUNDI WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. MBINU NI KUSAFIRI KWA NJIA YA  KIFICHO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAKABIDHIWE IDARA YA  UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO  KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA  MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA WAHAMIAJI HARAMU ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]
MNAMO TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 08:30HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MAJENGO KIJIJI CHA LUPA WILAYA YA CHUNYA   MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA LYIDIA D/O AMBAKISYE, MIAKA 25,  KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA LUPA  AKIWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI[GONGO] UJAZO WA LITA 5. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO]  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
MNAMO TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 09:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MAGUNGA KIJIJI CHA MAMBA WILAYA YA CHUNYA   MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA JOHN S/O LUTIMBO, MIAKA 29, MSUKUMA, MKULIMA, MKAZI WA MAMBA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 4. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO]  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
 [DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

No comments:

Post a Comment