
Waziri wa
Ujenzi (katikati) akiongozana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi
Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) na Eng. Mashaka Mgallah ambaye ni Meneja
wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mkoa wa Kigoma, kukagua eneo
lililokuwa kambi ya ujenzi wa barabara ya Mwandiga – Manyovu mkoani
Kigoma. Nyumba hizo zimetelekezwa kwa miaka 2. Wengine katika picha ni
Watendaji kutoka Taasisi mabli mbali za Serikali

Moja ya nyumba zilizotelekezwa katika kambi ya ujenzi wa barabara ya Mwandiga – Manyovu.

Waziri wa
Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Meneja
wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Eng. Mashaka Mgallah (wa pili kulia)
wakati alipofanya ziara ya ghafla kukagua nyumba katika kambi iliyokuwa
ikitumiwa na Wahandisi wakati wa ujenzi wa barabara ya Mwandiga –
Manyovu mkoani Kigoma.
Waziri wa
Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kukabidhiwa mara
moja kwa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma nyumba zote 13 zilizoko katika
kambi iliyokuwa ikitumiwa na Wahandisi waliosimamia ujenzi wa barabara
ya Mwandiga hadi Manyovu ambayo ujenzi wake umekamilika kwa kiwango cha
lami.
Hatua
hiyo ya Waziri Magufuli imetokana na nyumba hizo kuachwa bila ya
matumizi yoyote kwa muda wa miaka miwili. Akimhoji Meneja wa Wakala wa
Majengo wa mkoa wa Kigoma sababu za kuachwa kwa nyumba hizo kwa kipindi
chote hicho wakati yapo mahitaji makubwa ya nyumba kwa ajili ya
Watumishi wa Umma na Ofisi za Serikali, Meneja wa TBA wa mkoa huo Eng.
Mashaka Mgallah alibainmisha kuwa awali Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)
uliarifiwa kuwa majengo hayo yamekabidhiwa kwa Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Kigoma.
Katika
hali ya kusikitisha wakati Mheshimiwa Magufuli alipofanya ukaguzi wa
kushitukiza katika eneo hilo alikuta nyumba hizo zikiwa zimetelekezwa
huku vifaa vingi vikiwa vimeibwa vikiwemo viyoyozi na samani mbali
mbali. Kutokana na hali hiyo yakatolewa amelekezo kwa taasisi zote
zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi kutekeleza zoezi maalum la kuhakiki
mali zote zilizo katika miradi inayoendelea ili zithaminiwe mara miradi
hiyo inapokamilika tayari kwa kukabidhiwa Serikalini.
"Ninawaagiza
hasa Watendaji Wakuu wa Tanroads, TBA na TEMESA na Taasisis nyingine
katika Wizara ya Ujenzi mfanye ukaguzi wa mali zilizo katika kila mradi
unaoendelea nchi nzima ili pale mradi unapokamilika ifanyike tathmini ya
mali zinazokabidhiwa Serikalini" alisitiza Waziri Magufuli.
Naye
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kigoma ACP Frasser Kashai kwa upande wake
ameshukuru Waziri wa Ujenzi kwa uamuzi huo ambao ameuelezea kutolewa
katika wakati muafaka hasa kutokana na kuwepo kwa tatizo kubwa la makazi
kwa ajili ya askari wa jeshi hilo sio tu katika mji wa Kigoma bali
katika mkoa mzima kwa ujumla wake.
"Nyumba
hizo mnapewa bila ya malipo yoyote kwa ajili ya matumizi ya jeshi la
polisi hadi hapo taarifa nyingine itakapotolewa, TBA na Tanroads
wahakikishe kuwa huduma za maji na umeme zimeunganishwa katika eneo
hilo" alimalizia Waziri Magufuli.

No comments:
Post a Comment