Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, December 4, 2013

ABDULRAHMAN KINANA APOKEA KERO ZA WAFANYAKAZI TAZARA MBEYA


1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi huku wakiwa wameshika mabango ya kupongeza serilkali na Chama cha mapinduzi kwa kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya Chama cha hicho wakati alipopokelewa eneo la Iwambi akitokea Wilaya ya Mbeya Vijijini ambapo leo ameanza ziara katika wilaya ya Mbeya mjini na kutembelea Shirika la TAZARA na kuongea na wafanyakazi, ambapo amepokea matatizo mbalimbali ya shirika hilo na wafanyakazi, Katika ziara hiyo kinana ameongozana na Nape Nnauye Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Mbunge wa kuteuliwa , Kulia ni Ephraim Mwaitenda Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbeya mjini, Ndugu Abdulrahman Kinana na msafara wake anatarajia kurudi Dar es salaam kwa kutumia treni hiyo ya TAZARA mara baada ya kumalizika kwa zara yake mwishoni mwa wiki hiii .PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MBEYA2Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kulia akiwasili kwenye stendi kuu ya TAZARA mjini Mbeya wakati alipozungumza na wafanyakazi wa shirika hilo na kupokea kero  mbalimbali za shirika hilo na wafanyakazi wake, Kutoka kulia ni Ephraim Mwaitenda Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbeya mjini, Dr. Norman Sigalla Mkuu wa wilaya ya Mbeya na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki.3Baadhi ya wakuu wa vitengo mbalimbali wa shirika la TAZARA Mbeya wakimsubiri Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Meneja wa TAZARA wa Kanda ya Mbeya Bw Jija Nyirenda mara baada ya kupokelewa katika kituo hicho, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigalla.6Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kulia  Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigalla na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Mbunge wa kuteuliwa wakiingia kwenye ukumbi wa mkutano na wafanyakazi wa TAZARA11Baadhi ya abiria wakivinjari katika kituo hicho kulia anayepishana nao ni Nape Nnauye12Meneja wa TAZARA Kandaya Mbeya akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM ili kuongea na wafanyakazi wa shirika hilo.13Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiingia ukumbini huku akiongozana na Meneja wa TAZARA kanda ya Mbeya Bw. Jija Nyirenda14Baadhi ya wafanyakazi wa TAZARA wakimsikiliza katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana15Mwakilishi wa wafanyakazi wa shirika hilo Shaban Malekela akisoma taarifa ya wafanyakazi hao iliyoainisha matatizo yao wanayokumbana nayo katika shirika hilo.16Mfanyakzi mstaafu wa TAZARA Mzee  Seif Rashid akitoa kero katika mkutano huo.17Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanyakazi wa TAZARA 20Mkutano ukiendelea21Nape Nnauye akitoka kwenye ukumbi wa mkutano mara baada ya kumalizika kwa mkutano.22Abdulrahman Kinana akizungumza na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya wakati wakitoka kwenye mkutano huo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigalla.23Kituo kikuu cha TAZARA Iyunga mjini Mbeya

No comments:

Post a Comment