KATIKA makala iliyopita tuliona jinsi mwili unavyoweza kujitibu wenyewe ukipata mlo sahihi. Leo tunapenda kuzungumzia faida za nazi,
ambazo zinatokana na kuwa na mchanganyiko maalum wa aina nyingi za
mafuta zijulikanazo kama ‘medium chain triglycerides’ au kwa kifupi
(MCT’s).
Nazi
ikiliwa na binadamu hugeuza aina hizo za mafuta kuwa tindikali ambayo
kitaalamu huitwa ‘medium chain fatty acids’ au kwa kifupi (MCFA’s)
ambazo huua na kutokomeza virusi vya aina mbalimbali mwilini.
Tui la nazi
Matumizi ya nazi kama tiba kwa waathirika wa virusi duniani yalilipuka
kwa kasi mwaka 1990 mara baada ya mtafiti wa tiba kutoka Iceland, Bw.
Halldor Thormar, kubaini maajabu ya tiba hii.
Waathirika wa virusi vya aina mbalimbali duniani waliotumia nazi walitoa
ushuhuda wao wa namna walivyopata nafuu mara baada ya kutumia nazi kama
tiba. Licha ya kuponya maradhi waliyokuwa nayo, iliwaboreshea afya zao
na kuonekana kana kwamba si waathirika tena.
Dozi
yake ni rahisi, unywaji wa glasi nne za tui la nazi kwa siku au vijiko
sita vya mafuta ya nazi kila siku kwa muda wa kati ya miezi mitatu hadi
minne, huweza kuondoa maradhi yote yanayosababishwa na virusi mwilini na
pia kung’arisha ngozi na kuifanya kuwa nyororo.
Ushahidi wa faida ya nazi kama urembo upo kwa mabinti wa Kizaramo
wanaowekwa ndani na kuchuliwa mwili mzima kwa machicha ya nazi kwa miezi
kadhaa, ambapo wanapotoka nje huonekana warembo wenye ngozi nyororo
waliyoipata kiasili bila kutumia ‘krimu’ au mafuta mengine ya gharama.
Kama sote tujuavyo, virusi vya Ukimwi hudhoofisha kinga ya mwili. Mwili
unapokosa kinga hushindwa kuzuia virusi vya aina nyingine kukushambulia.
Kwa kawaida tiba ya virusi huwa ni zile dawa zenye uwezo wa kushambulia
virusi (antiviral), bakteria (antibiotic) na zile za kushambulia
fangasi (antifungus).
Hata
hivyo, dawa hizo ni kali sana kiasi cha kuwaumiza watumiaji na huwa na
madhara (side effects) zinapotumiwa kwa muda mrefu, ukiachilia mbali
gharama zake ambazo mwathirika mwenye kipato cha chini hawezi kuzimudu.
Lakini
unaweza kujitibu maradhi yatokanayo na virusi kwa njia rahisi na
salama. Kula nazi kwa wingi kadiri uwezavyo, kama ni muathirika basi
anza kunywa tui la nazi glasi nne kwa siku na utaona maajabu ndani ya
miezi mitatu tu. Kama tayari una vidonda visivyopona basi paka mafuta ya
nazi kila utokapo kuoga, na matokeo utayaona bayana.
Hata
hivyo tunajua kuwa si watu wote wako kwenye mazingira ya kupata nazi
kirahisi au kupata nazi bora yenye virutubisho vinavyotakiwa. Hivyo
tunawaomba msisite kuwasiliana nasi tuwape maelekezo ya kupata nazi bora
na mafuta yake au bidhaa zingine zenye dhamana ya kulinda afya zetu
kupitia lishe. Kwa ushauri, maoni, tafadhali wasilina nasi kupitia namba
za simu hapo juu.
No comments:
Post a Comment