ZAIDI ya familia 30 za wakazi wa kijiji cha Kasense nje kidogo ya Manispaa ya Sumbawanga, wamekosa pahala kuishi baada ya nyumba zao kubomolewa na nyingine kuezuliwa mapaa kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha.
Mvua
hiyo iliyonyesha juzi kuanzia saa 9 alasiri na ilidumu kwa saa mbili
huku upepo huo ukiangusha miti na kuwatia hofu wakazi wa kijiji hicho.
Diwani
wa Kasense, Cretus Jumbe, alisema mvua hiyo pia iliharibu madarasa
matatu na nyumba mbili za walimu katika shule ya Msingi Kasense ambazo
nazo ziliangukiwa na miti kwenye mapaa yake.
Jumbe
alisema hadi sasa kuna takriban nyumba 32 zilizopata madhara hayo
ambapo familia zote zimehifadhiwa kwa ndugu na jamaa zao wakisubiri
msaada zaidi toka serikalini.
Mkururugezni
wa Manispaa ya Sumbawanga, William Shimwela, ambaye alifika eneo hilo
muda mfupi baada ya maafa hayo, alisema timu ya wataalamu inatarajiwa
kufika leo kufanya tathmini ya maafa na kuangalia ni msaada upi wa
haraka unatakiwa.
“Tutakaa
na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ambaye ni Mkuu wa wilaya ili kuona
hatua zingine zinazofuata kwani tayari tumejionea hali halisi ya
wananchi walivyoathirika kutokana na tukio hilo na wanahitaji msaada wa
haraka kwa sababu hawana sehemu za kuishi,” alisema Shimwela.
Alisema madarasa yaliyoharibika yanahitaji ukarabati kabla ya Januari mwakani, ili wanafunzi waweze kuendelea na masomo.

No comments:
Post a Comment