WILAYA YA MBARALI – KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MNAMO
TAREHE 02.12.2013 MAJIRA YA SAA 07:50HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
KIJIJI CHA LEMBUKA- IYAMBOGO, KATA YA CHIMALA, TARAFA YA ILONGO WILAYA
YA MBARALI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIWAKAMATA
1. BERETE S/O TEFRA, MIAKA 24, 2. SAMWEL S/O GIRMA, MIAKA 30 NA 3.
MUATU S/O BALAGALA, MIAKA 23 WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA
WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. MBINU NI KUSAFIRI KWA NJIA YA
KIFICHO.
TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WAKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA
MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA
RAIA WA KIGENI ILI UCHUNGUZI DHIDI YAO UFANYIKE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAO IKIWA NI PAMOJA NA KUKAMATWA.
[BARAKAEL MASAKI - ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment