Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Johari Masoud Sururu kuwa Kamishna mpya wa Uhamiaji Zanzibar.
Kabla
ya uteuzi huu ambao unaanzia tarehe 24 Novemba, 2013 Bwana Sururu
alikuwa Mwambata wa Uhamiaji katika Ubalozi wa Tanzania jijini Abu
Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E).
Kufuatana na uteuzi huu, aliyekuwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Bwana Mwinchumu Hassan Salim sasa atapangiwa kazi nyingine.
Imetolewa na:
Isaac J. Nantanga
MSEMAJI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
04 Desemba, 2013
No comments:
Post a Comment