Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, December 4, 2013

Taarifa ya Chadema mkoa wa Arusha baada ya ofisi kuchomwa moto

.....
Matukio yanayokiandama Chama cha Demokrasia na Maendeleo[CHADEMA]yamezidi kuchukua nafasi ambapo mkoani Arusha watu wasiojulikana wameshutumiwa  kuchoma moto ofisi za chama cha hicho  Jumanne tar 03dec 2013 asubuhi  na kusababisha uharibifu mdogo.
CHADEMA
katibu wa Chadema mkoa wa Arusha Mchungaji Amani Golugwa amesema ‘Mpaka hivi sasa tunavyoongea eneo la ofisi ndani ya ofisi kabisa eneo la bafu na choo sling boad yote imeungua na upande wa juu ya bati umeungua na kikubwa zaidi walitaka kuingia chumba cha computer room ambacho tunahifadhi data kwa wanachama wetu kwa kanda nzima ya kaskazini,majimbo 33,sasa baada ya kushindwa hiyo ndo wakatengeneza shoti ya umeme pakashika moto,tunamshukuru Mungu tu kwamba huu moto haukuendelea sana kwa hiyo athari haipo kwenye nyaraka zozote wala kwenye machine zilizopo hapa ofisini’.attac.hment
‘Ni sling board pekeyake iliyoungua pamoja na upande mmoja ambapo kuna bafu na choo ndipo palipoungua lakini ni kweli jambo hili limetokea’.
‘Ni mapema mno kulizungumzia hasa kuliunganisha na kinachoendelea saivi kwenye chama lakini hisia zetu za ndani zinatupeleka mahali fulani ambapo bado ni mapema kulielezea lakini ni tukio ambalo limetufedhehesha na kutushangaza hasa lengo lilikua ni kuiunguza ofisi yote iungue kabisa,bila kujali majirani waliopo hapa na vitu vya thamani hasa hizo data zilizopo kwenye mashine zetu japo hua tunafanya back up ya kila siku lakini ni kitu ambacho kimetushtua sana’.
‘Ukweli yanayoendelea sasa hivi watu wengine wanaweza wakatafsiri ni migogoro ndani ya chama,lakini ukweli ni kwamba chama kinajisafisha chama kinatumbua majipu nitumie kauli hii,kama mtu mwilini una majipu hamsini huwezi ukasema utumbue majipu mawili au matatu uyaache useme umepona utayatumbua yote,kwa hivyo kinachoendelea saivi ni bundi ametua chadema,ni bundi anafukuzwa kwa hivyo tuna mambo mengi yanayokuja na kwa uzoefu wangu wa kisiasa ninaelewa kwamba zoezi tunalolifanya sasa hivi la kushughulikia wahaini,wasaliti linaeza kuwa la maumivu kwa wale ambao walikua na nia mbaya na malengo mabaya ndani ya chama kwa saababu mpango wao umeshindwa,kwa hivyo ninaweza kujikuta kama kiongozi kuna vitu fulani naviwaza na kuviangalia kwenye sura ya kimkakati’.

attachment

No comments:

Post a Comment