JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Mhe. Rais
Tume
ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi na wadau
wengine kuwa hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Dkt. Ali
Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
itafanyika siku ya Jumatatu, Desemba 30, 2013 saa 6:00 mchana katika
Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Hafla
hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na Viongozi wa Serikali, Vyama vya
Siasa, Taasisi za kidini, Asasi za kiraia na wananchi wa kawaida.
Mwenyekiti
wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba anatarajia kuwakabidhi Waheshimiwa
Marais, ripoti ya mchakato wa Katiba na rasimu ya Katiba.
Rasimu
hiyo ya Katiba imetokana na maoni ya wananchi, viongozi na makundi
mbalimbali waliyowasilisha kwa Tume kupitia njia mbalimbali zikiwemo
mikutano, barua pepe, anuani za posta, tovuti (www.katiba.go.tz) na ukurasa wa facebook wa Tume (Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania).
Imetolewa na:
Assaa Rashid,
Katibu,
Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
Dar es Salaam
Disemba 27, 2013.
No comments:
Post a Comment