MSANII Victor Peter kutoka Bongo Movie afariki dunia kwa kujinyonga katika gest moja iliyotambulika kwa jina la SAFARI JUNIOUR ilioko maeneo ya Kisosora huko mkoani Tanga.
Hapo pichani ni mwili wa marehemu ulivyokuwa ukipakiwa katika gari kupelekwa katika hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo,
Chanzo cha habari kiliieleza kuwa msanii huyo alikuwa katika harakati zake za kushoot filamu yake mpya ambayo alicheza kama muhusika mkuu katika filamu hiyo.
Kilichowashangaza wenzake ni kwamba filamu iliisha jana Jumatatu 27/01/2014 na story ilimalizikia Vicktor kufa kwa
kujinyonga matokeo yake leo alfajiri Victor akakutwa amejinyonga kweli
na kuiaga dunia, Mpaka sasa chanzo cha kifo chake bado hakijatambulika.
No comments:
Post a Comment