Ndugu
zangu waandishi wa habari, nimewaiteni hapa kwa dharura, ili kuweza
kuwafahamisha hali halisi ya mauaji yaliyotokea katika siku za hivi
karibuni katika mkoa wa Kipolisi wa Tarime Rorya. Mnamo tarehe 26
Januari, 2014 majira ya saa 12.00 asubuhi huko katika kijiji cha Mogabiri
katika mkoa wa kipolisi Tarime Rorya, jambazi asiyefahamika kwa jina aliwaua kwa risasi Zakaria Mwita Marwa miaka 28 na Erick Lucas Maranya miaka 24 baada ya kukutana nao njiani. Siku hiyohiyo, majira
katika mkoa wa kipolisi Tarime Rorya, jambazi asiyefahamika kwa jina aliwaua kwa risasi Zakaria Mwita Marwa miaka 28 na Erick Lucas Maranya miaka 24 baada ya kukutana nao njiani. Siku hiyohiyo, majira
ya saa 4:00 usiku, katika kijiji hichohicho cha Mogabiri, jambazi huyo
alimuua Robert Kisiri miaka 45 baada ya kuvamia Grocery inayomilikiwa na
Chacha Ryoba na kumjeruhi mtu mwingine mmoja. Tarehe 27 Januari, 2014 majira ya 11:30 alfajiri katika kijiji cha Mugabiri, jambazi huyo alifanya mauaji tena kwa kumpiga risasi David Mwasi Matiko miaka 39 na kumpora simu yake aina ya Nokia. Katika tukio hilo, pia, alimjeruhi Machungu Nyamahemba miaka 19 ambaye bado amelazwa katika hospitali ya Tarime kwa Matibabu.
Siku
hiyohiyo ya tarehe 27 Januari, 2014 majira ya saa 2:00 usiku katika
kijiji cha Nkende, jambazi huyo alimuua kwa kumpiga risasi Juma Marwa
Nyaitara miaka 30. Baada ya kufanya mauaji hayo, jambazi huyo aliwapora
simu zao za mkononi Chacha Magige na Masero Marigiri wote wa kijiji cha
Nkende. Usiku wa kuamkia tarehe 28 Januari, 2014, jambazi huyo aliendelea kuua watu wengine watatu ambao bado majina yao hayajafahamika. Mtu mmoja alipigwa risasi wakati akiendesha pikipiki
katika kijiji cha Nkende na wengine wawili waliuawa baada ya kukutwa na
jambazi huyo wakiwa wanatengeneza gari lililokuwa limewaharibikia katika
kijiji cha Mogabiri.
Hadi sasa juhudi kubwa za kumsaka jambazi huyo zinaendelea kufanyika na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi. Aidha, mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernesti Mangu, ametuma timu maalum kutoka makao makuu ya jeshi la Polisi inayohusisha kamisheni ya Oparesheni, Upelelezi na Intelijensia kwenda kuongeza nguvu katika juhudi zinazofanyika na ngazi ya mkoa kuhakikisha kwamba, jambazi huyo anakamatwa upesi ili kuondoa hofu kwa
wananchi.
Jeshi
la Polisi nchini, linatoa wito kwa wananchi wote kutoa ushirikiano ili
jambazi huyo aweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria
haraka. Mwananchi mwenye taarifa za mhalifu huyo anaweza kutumia namba
ya simu ifuatayo 0754 785557.
Mkuu wa Oparesheni wa Jeshi la Polisi,
Kamishna Paul Chagonja
No comments:
Post a Comment