Jaji
Mstaafu Mark Bomani,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape
Nnauye na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)
Mh.Stephen Wassira ni miongoni mwa viongozi mbali mbali walioshiriki
mazishi ya kada maarufu ambaye pia alishawahi kuwa Mkuu wa Wilaya katika
Wilaya mbalimbali nchini.
Mama
Anna Mkapa,Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna
Tibaijuka na Mwenyekiti wa CCM Moshi Mjini Elizabeth Minde wakiwa
miongoni mwa mamia ya Watanzania waliojitokeza kumzika kada wa siku
nyingi Deusdedit Mtambalike.
Waombolezaji wakiwa kwenye nyuso za huzuni wakati wa mazishi ya mpendwa wao Deusdedit Mtambalike.
Sala
ya kumuombea Marehemu Deusdedit Mtambalike aliyefariki tarehe 15 Januari
2014 nchini Afrika ya Kusini ilisomwa nyumbani kwake kabla ya Mazishi.
Wanandugu wa Marehemu Deusdedit Mtambalike wakiwa wamebeba mashada ya maua .
Mwanasiasa
wa siku nyingi na ambaye alishawahi kushika nyazfa mbalimbali za
serikali Balozi Paul Rupia akitoa salaam za pole kwa familia ya marehemu
Deusdedit Mtambalike na kumuelezea marehemu kama mtu aliyemwema na
asiyechoka kushauri kwenye jambo lolote alotakiwa kushauri.
Jaji
Mstaafu Mark Bomani akimuelezea marehemu Deusdedit kama mtu ambaye
hakusita wala kuwa na woga katika kuzungumzia jambo lenye manufaa kwa
jamii.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa salaam za rambirambi kwa
niaba ya CCM Makao Makuu wakati wa mazishi wa aliyekuwa Kada wa Chama
Cha Mapinduzi Marehemu Deusdedit Mtambalike.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais(Mahusiano na Uratibu) Mheshimiwa Stephen Wassira
akitoa salaam za pole kwa niaba ya Serikali kwenye mazishi ya Ndugu
Deusdedit Mtambalike yaliofanyika nyumbani kwa marehemu Kimara Bonyokwa.
Watoto
wa Marehemu Deusdedit Mtambalike wakiwa wenye nyuso za simanzi na
huzuni pamoja na Mama yao na Ndugu wa karibu wakati wa sala ya mwisho
kabla ya mazishi ya Baba yao mpendwa.
Sehemu ya watu waliojitokeza kwenye mazishi ya Deusdedit Mtambalike
Profesa Mahalu akiweka mchanga kama ishara ya kumzika rafiki yake Marehemu Deusdedit Mtambalike
Mke wa Marehemu Deusdedit Mtambalike akiweka shada la maua juu ya kaburi .
Watoto
wa marehemu wakiweka shada la Maua kwenye kaburi la baba ya mpendwa
Marehemu Deusdedit Mtambalike aliyefariki dunia tarehe 15 Januari 2014
nchini Afrika ya Kusini.
No comments:
Post a Comment