Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, January 27, 2014

MH;MWIGULU NCHEMBA AWASILI MKOA WA TANGA,AENDESHA KIKAO CHA WATENDAJI WA CHAMA MKOA WA TANGA

Naibu Katibu Mkuu(Kulia) Mh Mwigulu Nchemba akisikiliza Utambulisho wa Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga wanaotambulishwa na Katibu wa Mkoa wa Tanga wa CCM,Kshoto ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mh;Mrisho Gambo.
Watendaji wa Mkoa wa Tanga wa Chama Cha Mapinduzi wakitoa zawadi ya Mbuzi kwa Naibu Katibu Mkuu kwa Kuteuliwa kwake kuwa Naibu waziri wa Fedha,Hii inaonesha ni namna gani alivyomchapa kazi na anavyoaminika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh;Jakaya Mrisho Kikwete.
Zawadi zinaendelea kwa Mh:Mwigulu Nchemba kwa Kuteuliwa kwake kuwa Naibu waziri wa Fedha. Kikao kimeshaanza na Kinaendelea sasa,Naibu katibu Mkuu anatoa Ujumbe alioubeba kwa Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi hapa Mkoa wa Tanga.
*******
Naibu katibu Mkuu wa CCM Bara Mh;Mwigulu Nchemba hii leo 27/01/2014 asubuhi amewasili Mkoa wa Tanga akitokea Arusha kwenye Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi mdogo wa Udiwani kata ya Sombetini.Mh;Mwigulu Nchemba amekuwa kwenye ziara ya Kichama ya Kuzindua kampeni za Uchaguzi wa Udiwani kata mbalimbali Nchini,Akiwa ameanzia Mkoa wa Mtwara(Tandahimba),Mkoa wa Manyara(kiteto),Mkoa wa Arusha(Sombetini) na hii leo ameingia Mkao wa Tanga na Jioni ya Leo atakuwa Bagamoyo kwenye Uzinduzi wa Kampeni za Udiwani Kata Kibindu.
Naibu Katibu Mkuu licha ya kuendesha Ufunguzi wa Kampeni za Uchaguzi wa udiwani,Pia amekuwa akifanya Vikao vya ndani vya Mkoa husika anaofika kuzindua Kampeni.Vikao vya ndani vya Watumishi wa Chama Cha Mapinduzi vimewa vikihusisha Makatibu wa Mikoa na Wilaya na Jumuia zake zote.Ameshafanya Vikao hivyo Mkoa wa Mtwara,Manyara,Arusha,Hai,Moshi na hii leo ameshatua Tanga kwaajili ya Kikao hicho cha Watendaji wa Chama Mkoa wa Tanga.
 

Picha zote na Habari Kwanza Blog

No comments:

Post a Comment