Rais wa
Misri aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi anatarajiwa kufikishwa
mahakamani jumanne ikiwa ni moja ya mashtaka ya uhalifu yanayomkabili
kiongozi wa chama cha kiislamu.
Bwana
Morsi na zaidi ya wanachama 100 wa kundi lililopigwa marufuku la Muslim
Brotherhood wanakabiliwa na mashtaka kwa kutoroka jela mwaka 2011 na
shutuma za kuua polisi wakati wa mapinduzi ambayo yamemuondoa madarakani
kiongozi wa muda mrefu Rais Hosni Mubarak na kumuingiza madarakani
bwana Morsi.
Washtakiwa
wengi wametambuliwa kuwa ni wanachama wa kundi la wanamgambo wa
kipalestina la Hamas, kundi la wanamgambo la Hezbollah lenye makao yake
nchini Lebanon na kikosi cha Revolutionary Guard cha Iran.
Bwana
Morsi na wanachama wengine waandamizi wa kundi la Brotherhood pia
wanakabiliwa na mashtaka kwa shutuma za kuchochea mauaji ya waandamanaji
wa upizani wakati akiwa madarakani.
Rais huyo
wa zamani na watu wengine 35 pia watashtakiwa kwa shutuma za upelelezi
kwa kushirikiana na kundi la wapalestina la Hamas.
Jeshi la
Misri lilimuondoa mamlakani bwana Morsi mwezi July mwaka jana. Hosni
Mubarak aliondolewa madarakani kufuatia upinzani wa umma ambao ulianza
Januari mwaka 2011.
Chanzo ni voaswahili.com
No comments:
Post a Comment