KIKOSI
cha Usalama Barabarani na Jeshi la Polisi mkoani Pwani, wamepiga
marufuku kitendo cha madereva, makondakta wa mabasi, kushuka ndani ya
magari yao na kwenda kupeleka kadi za gari kwa trafiki kibandani, nyuma
ya gari ili ikaguliwe.
Agizo
hilo limelenga kuzuia ushawishi wa vitendo vya rushwa kwa baadhi ya
makondakta na madereva wa mabasi dhidi ya askari wa Kikosi cha Usalama
Barabarani.
Akizungumza
na Majira Mjini Kibaha, mkoani Pwani mwishoni mwa wiki, Kamanda Polisi
Kikosi cha Usalama Barabarani, mkoani humo, Nassor Sisiwaya, alisema
yapo malalamiko na hisia kwa baadhi ya watu kuwa, kondakta au dereva wa
basi anaposhuka kupeleka kadi kwa trafiki ikaguliwe, huwa anatoa
rushwa.
"Kuna
watu wanasema kadi anayoipelekwa kwa trafiki, huishikanisha na fedha
ambayo humpa trafiki kama rushwa ili asimchukulie hatua za kisheria
katika makosa ya usalama barabarani atakayokuwa ameyatenda.
"Ili
kuondoa mtazamo huo na vishawishi vya rushwa, nimepiga marufuku dereva
au kondakta kushuka ndani ya gari ili kumfuata trafiki badala yake
trafiki atapanda ndani ya gari, atakagua na kuuliza maswali hadharani
mbele ya abiria," alisema.
Alisema
askari wa Usalama Barabarani nchi nzima, wamekuwa wakilalamikiwa
wakidaiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa hivyo yeye hayapingi
malalamiko ya baadhi ya askari kuwa
na tabia za aina hiyo ila si askari wote.
Aliongeza
kuwa, asilimia kubwa ya askari wa Usalama Barabarani ni waadilifu ambao
wanatekeleza majukumu ya kazi zao na kusimamia sheria za barabarani
kikamilifu.
Kamanda
Sisiwayaalisema kama kuna trafiki mwenye ugonjwa wa kuomba na kupokea
rushwa, aiombe na kuipokea hadharani mbele ya abiria.
"Katika
Stendi ya Mabasi Maili Moja, Kibaha, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana
na Kamati ya Usalama Barabarani ya Mkoa, tutafunga spika kubwa na
kuwatangazia kondakta, madereva wasishuke katika magari yao wabaki ndani
na kukaguliwa mbele ya abiria wao," alisema.
Alisema
jeshi hilo halitamvumilia askari ambaye itabainika anajihusisha na
vitendo vya rushwa ambapo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake
pamoja na kufukuzwa kazi.
"Hatupo
tayari kuona sifa za jeshi letu zikichafuliwa na askari wachache kwa
tamaa ya pesa na kukiuka maadili ya kazi zao,viongozi tumejipanga
kikamilifu kuwasaka, kuwakamata kwa ushirikiano na wananchi,
tutamshughulikia ipasavyo ili iwe mfano kwa askari wengine," alisema.
MAJIRA.
No comments:
Post a Comment