· MABWENI MANNE YA SHULE YA SEKONDARI WENDA YATEKETEA KWA MOTO.
MTU MMOJA AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI.
MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA YONA KAIZA @ SIMKONDA (35) MKAZI WA KIJIJI CHA
YALA ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI KWA KUTUMIA SILAHA BUNDUKI AINA
YA GOBOLE NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. TUKIO HILO LILITUKEA MNAMO TAREHE
27.01.2014 MAJIRA YA SAA 03:30HRS BAADA YA WATU HAO KUFIKA NYUMBANI KWA
MAREHEMU NA KUPIGA HODI, MAREHEMU ALIPOFUNGUA MLANGO ALIPIGWA RISASI
KIFUANI NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO. HAKUNA KITU KILICHOCHUKULIWA,
JUHUDI ZA KUWATAFUTA WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI ZINAENDELEA. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA
KWA TUKIO HILI AZITOE ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
MABWENI MANNE YA SHULE YA SEKONDARI WENDA YATEKETEA KWA MOTO.
MABWENI
MANNE YA SHULE YA SEKONDARI WENDA YAMETEKETEA KWA MOTO NA KUSABABISHA
UHARIBIFU WA MALI. TUKIO HILO LILILOTOKEA TAREHE 27.01.2014 MAJIRA YA
SAA 20:15HRS HUKO MBALIZI FIDELIS DANIEL
(54) MKURUGENZI WA SHULE HIYO ALIGUNDUA KUUNGUA KWA MABWENI MANNE YA
SHULE HIYO WANAYOLALA WAVULANA KATI YA MABWENI HAYO MAWILI YAITWAYO
STATEHOUSE NA
MALCOM X YALITEKETEA KABISA KWA KUUNGUA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA VITANDA
74 WALIVYOKUWA WANALALIA WANAFUNZI NA VITU MBALIMBALI. AIDHA MABWENI
YAITWAYO KOFFI ANNAN NA MARCUS YALIUNGUA MOTO AMBAO ULIDHIBITIWA KWA
KUZIMWA. JUMLA YA WANAFUNZI 355 WALIKUWA WANAISHI KATIKA MABWENI HAYO.
CHANZO CHA AJALI HIYO BADO KUFAHAMIKA KWANI WAKATI TUKIO LINATOKEA
WANAFUNZI WALIKUWA MADARASANI. KATIKA TUKIO HILO HAKUNA MADHARA YA
KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA. THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA
BADO KUFAHAMIKA. MOTO ULIZIMWA KWA USHIRIKIANAO BAINA YA KIKOSI CHA ZIMA
MOTO NA UOKOAJI, JESHI LA POLISI, WANAFUNZI NA WANANCHI WA ENEO HILO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI
AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUCHUKUA TAHADHARI ZA MAKUSUDI
DHIDI YA MAJANGA YATOKANAYO NA MOTO KAMA KUHAKIKISHA KATIKA MAJENGO
KUNAKUWA NA VIFAA VYA KUZIMIA MOTO “FIRE EXTINGUISHER” NDOO ZA KUCHOTEA
MCHANGA NA MAJA, KUWEKA MIUNDO MBINU YA BARABARA ZINAZOWEZA KURAHISISHA
MAGARI YA KUZIMA MOTO NA UOKOAJI KUFIKA KATIKA MAENEO YA MATUKIO KWA
URAHISI.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment