Mkurugenzi wa Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Luteni Jenerali Sylivester Rioba akipokea msaada huo kwa niaba ya serikali kutoka kwa Balozi wa Mhe. Lu Youqin.
Na Eliphace Marwa-Maelezo
Ubalozi
wa China nchini Tanzania kwa kushirikiana na makampuni ya watu wa China
nchini wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko
mkoani Morogoro toka kwa Mhe. Lu Youqing ,vyenye thamani ya sh. milioni
30.
Msaada huo umetolewa na Balozi wa China nchini Tanzania Mhe.Lu Youqing na ulikabidhiwa kwaMkurugenzi wa Idara ya Maafa kutoka
Ofisi ya Waziri Mkuu, Luteni Jenerali Sylivester Rioba akipokea msaada
huo kwa niaba ya serikali amesema kuwa anaishukuru Serikali ya China
kwani imekuwa mstari wa mbele pale Tanzania inapopata maafa mbalimbali.
Aidha
Luteni Jenerali Rioba aliongeza kuwa mafuriko hayo ya aina yake
hayajawi kutokea yalianzia milima ya Kilosa na Mvomero na kupelekea
kufurika kwa mto Mkundi.
“Mheshimiwa
Balozi mvua hizi zilikuwa kubwa ambazo hazijawahi kutokea wilayani
Mvomero na kupelekea kuharibu daraja la Dumila ambalo ndiyo kiunganishi
cha Mkoa wa Morogoro na Dodoma,” alisema Luteni Jenerali Rioba.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe.Antony Mtaka akiongea kwa niaba ya Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro amesema kuwa mamia ya nyumba ikijumuisha madarasa,
majengo ya mahakama ya mwanzo, mashamba na barabara zimeharibiwa vibaya
na mafuriko hayo.
“Kwa
niaba ya Serikali napenda kushukuru Serikali ya China kupitia Mhe.
Balozi Lu kwa msaada huu na ningependa kuahidi kuwa msaada huu
utawafikia walengwa kama ilivyokusudiwa, ”alisema Mhe. Mtaka.
Kwa
upande wake Balozi wa china ametoa pole kwa waathirika wa mafuriko na
kusema kuwa watu wa Jamhuri ya China wako pamoja nao katika kipindi hiki
kigumu.
“China
na Tanzania ni marafiki wa muda mrefu hivyo kampuni ya ujenzi ya CCECC
ilichukua hatua za haraka katika kushiriki ujenzi wa daraja hilo kwa
kushirikiana bega kwa bega na ndugu zao Watanzania kwa kufanya kazi
usiku na mchana na kumaliza ujenzi huo kwa muda wa siku mbili,” alisema
Balozi Youqing.
Ubalozi
wa China kwa kushirikiana na makampuni ya China nchini umetoa vitu
mbalimbali ikiwemo Chakula, mashuka, madawa na maturubahi ikiwa ni
sehemu ya mchango wao kwa waathirika hao wa mafuriko mkoani Morogoro.



No comments:
Post a Comment